Wema Sepetu Amezua Timbwili lenye Ujazo Ndani ya Gereza la Segerea
WEMA Isaac Sepetu ‘Pedeshee’, amezua timbwili lenye ujazo ndani ya Gereza la Segerea, Dar es Salaam alipokwenda kuwatembelea mastaa wenzake walio nyuma ya nondo kwa misala tofauti, Kajala Masanja na Elizabeth Michael ‘Lulu’. Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita Juni 2, mwaka huu ambapo Wema alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutifuana na maafande wa magereza hadi akapigwa marufuku kukanyaga tena eneo hilo. Chanzo hicho kilidai kuwa Wema alifika gerezani hapo akiwa amesheheni mazagazaga kibao ya ‘mazawadi’ ya mashosti zake hao, jambo lililowashtua maafande wa magereza na baadhi ya ndugu na jamaa wa mahabusu wengine waliokuwa wamekwenda kuwatembelea ndugu zao. UKAGUZI Ilidaiwa kuwa baada ya kuwafikia maafande hao walimuomba Wema kabla hajakabidhi zawadi hizo kwa Kajala na Lulu wazikague. Iliendelea kusemekana kwamba, wakati zoezi hilo linafanyika, ndipo mwigizaji huyo alipoanza kulalamika kucheleweshwa huku askari nao wakihoji kwa nini alinunua vitu vyote hivyo mbali badala ya kununua mahali hapo. Chanzo hicho kilisema kuwa katika kurushiana maneno huku bangi ikitajwa ndipo kukatokea kufokeana, Wema akisisitiza kuwa wampishe akawaone rafiki zake. Ilielezwa kuwa mzozo huo ulichukua dakika kadhaa ambapo Wema alichimba mkwara ndipo akapigwa marufuku kukanyaga gerezani hapo na kushindwa kuwaona Lulu na Kajala. BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA Risasi Mchanganyiko lilizungumza na Wema ili kupata ukweli wa ishu hiyo ambapo mbali na kukiri, alikuwa na haya ya kusema: “Walisema eti kisa nilienda na vitu ambavyo sikununua pale. Ukweli ni kwamba vile vitu nilinunua pale Namanga (Dar). Hata nashindwa kuelewa kama kweli hilo ni kosa linaloweza kuwafanya kunizuia kwenda kuwatembelea rafiki zangu tena.”