SNURA:WEMA KANIFANYA NICHUKIWE KINOMA
SHOSTI namba moja wa msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Snura Mushi ameeleza kuwa, tangu amekuwa karibu na staa huyo amejikusanyia maadui wengi bila kujua sababu.
Snura aliyasema hayo hivi karibuni kwenye televisheni moja jijini Dar wakati alipokuwa akizungumzia ishu ya kwamba yeye amegeuka kuwa bodigadi na mbeba mabegi wa Wema.
Alisema, yeye na Wema ni marafiki walioshibana na wamekuwa wakisaidiana katika mambo mengi lakini anashangaa kuona anachukiwa na watu.
“Inaniuma sana, eti watu wanasema mimi ni mbeba mabegi na simu za Wema, wengine wanasema mimi ni bodigadi wake. Mbaya zaidi wanafikia hatua ya kunizushia mabaya na kunichukia bila sababu,…kwa kifupi inanichoma ila