Bongo Movies News: Husna Idd (Sajenti) Asusiwa Siku ya Birthday yake
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitutonya kuwa, katika sherehe hiyo Sajenti alitarajia kupata kampani kubwa kutoka kwa wasanii wenzake hao lakini ikawa tofauti na matarajio yake.
“Alifanya sherehe pale nyumbani kwao na alitarajia wasanii wa Bongo Movie kuhudhuria lakini hakuonekana hata mmoja hali iliyosababisha pati idorore,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kujua sababu za msanii huyo kususiwa sherehe yake, mwandishi wetu alimtafuta Sajenti na alipopatikana alisema:
“Kweli nilifanya ‘bethdei’ na siyo mimi niliyeandaa, niliandaliwa na marafiki zangu wengine akiwemo Jack wa Maisha Plus na sikuwa na taarifa kwani walinifanyia sapraizi, hivyo siyo kweli kuwa wasanii wenzangu walinisusia. Yaani mimi Husna nisusiwe? Hiyo haitatokea.”