|

UWOYA: WOLPER KANIROGA


Na Imelda Mtema
IRENE Uwoya amefungua ukurasa mpya wa bifu kati yake na staa mwenzake wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper baada ya kudai kuwa mwenzake huyo si bure atakuwa kamroga.
Uwoya alifunguka hayo akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro ‘KIA’ mkoani Kilimanjaro alipokwenda kwa ajili ya shughuli za uzinduzi wa filamu ya msanii mwenzake, Single Mtambalike ‘Richie’.
Kisa cha Irene kusema hivyo ni baada ya staa huyo pamoja na wengine kufanyiwa utambulisho na mwandaaji wa Miss Kilimanjaro, Brian Kikoti kwa waandishi na wageni wengine kisha jina lake kukosewa.
Kikoti aliwatambulisha mastaa hao na kulichanganya jina la Uwoya kwa kumtaja kama Jacqueline Wolper kitendo kilichomshitua.
Kabla ya kufika kwa Uwoya, mwandaaji huyo aliwatambulisha wasanii wengine kwa ufasaha lakini alipofika kwa staa huyo akatereza na kulitaja jina la Jacqueline Wolper kitu kilichomshtua na kumkasirisha Uwoya.
“Kuna nini jamani? Wolper atakuwa kaniroga, haiwezekani, hii si bure, huyo anasafiria jina langu kwa kuwa hii si mara ya kwanza,” alisema Uwoya huku akirejea kitendo cha Mtangazaji wa Runinga ya Clouds ya jijini Dar, Zamaradi Mketema ambaye naye aliwahi kumwita Jacqueline Wolper wakati alipokuwa akimhoji.

Posted by Unknown on 11:37 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added