Mwape atupiwa virago Jangwani
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesitisha rasmi mkataba wake na mshambuliaji wao wa kimataifa, Devis Mwape huku vifaa vyao vipya vya kimataifa vikitua klabuni hapo leo kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Kagame, michuano inayoanza kutimua vumbi Julai 14 jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Celestine Mwesigwa alisema wameamua kuachana na mchezaji huyo na kumuongezea mkataba beki Shadrack Nsajigwa kutokana na uzoefu wake kwenye klabu hiyo.
Nsajigwa alielezwa kujiunga na Gor Mahia ya Kenya baada ya kuwapo taarifa kuwa alikuwa na mpango wa kuachwa katika klabu hiyo.
Katibu wa Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali alisema klabu yao mwaka huu imeamua kusajili wachezaji chipukizi wenye uwezo. Alisema pia kuwa wachezaji wa nje wameshamalizana.
Awali ililipotiwa kuwa wachezaji ambao wanatarajia kuachwa ni Mwape, Yaw Berko na Kenneth Asamoah.
Yanga imeanza mazoezi jana chini ya kocha wao msaidizi Felix Minziro kwa ajili ya Michuano ya Kagame.