|

Master Jay Na Mwimbaji wa Kike Shaa Waachana



Na Mwandishi Wetu
WAPENZI masupastaa ambao iliwahi kuelezwa kwamba wanapendana sana, Joachim Kimaryo ‘Master Jay’ na Sarah Kaisi ‘Shaa’, wanadaiwa kumwagana rasmi.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa tofauti za kimapenzi kati ya Jay na Shaa, zimesababisha mpaka kuyumba kwa uhusiano wao wa kikazi ambao walikuwa nao kwa muda mrefu.
Tangu Shaa alipoibuka kimuziki na baadaye alipojitenga na Kundi la Coca Cola Pop Star, alikuwa akisimamiwa kimuziki na Jay kwenye lebo yake ya MJ Records.
Habari kutoka kwa chanzo chetu, zimedai kuwa baada ya kugombana na Jay, sasa hivi Shaa amehamia kwenye menejimenti mpya chini ya Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Hamis Taletale ‘Babu Tale’.
“Hivi sasa kazi zote za muziki, Shaa anafanya chini ya Babu Tale. Kweli mapenzi ni mchezo wa ajabu, wapendanao wanaweza kuwa maadui,” kilisema chanzo chetu.
Shaa hakupatikana kufafanua hilo, lakini Jay alisema: “Sina tofauti yoyote na Shaa na sijagombana naye. Uhusiano wetu upo vizuri ila nimemruhusu asimamiwe na Tale kwa sababu nahitaji apate usimamizi na uangalizi wa karibu zaidi.
“Mambo mengine nitaendelea kumfanyia, ila umeneja ndiyo nimeamua kumuachia Tale, nikiamini sasa Shaa atakuwa vizuri sokoni. Tale anaweza kumsimamia vizuri.”
Babu Tale alipopatikana kuzungumzia kuhusu kuanza kumsimamia Shaa, alikiri na kuongeza: “Hapa ieleweke kuwa Shaa hatakuwa Tip Top, nitamsimamia kimuziki kama msanii wa kujitegemea.”
Alipoulizwa kuhusu yeye kuwa chanzo cha ugomvi kati ya Shaa na Jay, Tale alijibu: “Hapana, hiyo haipo kabisa. Mimi namsimamia kimuziki tu, nachojua kuhusu Shaa na Master Jay bado ni wapenzi na wanapendana sana lakini siwezi kuzungumza kiundani kwa sababu hayo ni mambo yao binafsi.”
Source

Posted by Unknown on 12:18 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added