|

Makocha ndani waisusia Yanga

 BAADHI ya makocha wa soka nchini wameanika sababu zinazowafanya kutojitokeza kuomba kazi ya kukinoa kikosi cha Yanga msimu ujao.

Yanga  kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kumtafuta mrithi wa kocha Kostadin Papic aliyemaliza mkataba wake msimu uliomalizika.

Pamoja na kutoa nafasi kwa makocha wa hapa nchini kujitokeza kuomba nafasi hiyo, lakini ni makocha kutoka mataifa ya nje tu waliojitokeza.

Akizungumzia kitendo cha makocha wa ndani kushindwa kujitokeza kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda alisema tatizo kubwa la viongozi wa soka hapa nchi ni kuamini kocha wa kigeni pekee ndiye mwenye uwezo.

"Tatizo ni moja moja tu viongozi wa klabu zetu akili zao kwamba makocha wa nje ni bora  na sisi wanatudharau, lakini ni mimi huyu huyu ndiye niliyewafukuza Kondic(Dusan), Papic na Timbe (Sam) baada ya kuwafunga na JKT Ruvu yangu."

"Siwezi kujipeleka kuomba kazi Yanga kwani itakuwa ni sawa na kujiuza, mimi najiamini nina uwezo mkubwa unaolingana na hata kuwazidi hao wa nje."
Naye kocha wa zamani wa timu ya  Ashanti United na  Bandari Mtwara, Kenedy Mwaisabula alisema kuwa kujiamini katika kazi zake na msongamano wa majukumu ndiyo sababu kuu inayomfanya asiombe jukumu hilo.

"Nimewahi kufundisha timu karibu tano za Ligi Kuu, lakini na zote hizo sijawahi kuomba kazi, wao ndio huwa wananifuata kwa sababu naamini uwezo wangu hivyo sina sababu ya kujipeleka.

Kwa upande Sekilojo Chambua ambaye licha ya kuwa na taaluma ya ukocha pia amewahi kuichezea Yanga siku za nyuma, alisema: "Sijui chochote kuhusu vigezo wanavyotumia wala mchakato wenyewe unavyoendeshwa.

"Ningekuwa nafahamu angalau kidogo mchakato wenyewe ningekuambia kwanini mimi  na wengine hawajajitokeza licha ya wengine kuwa wanavigezo."

Posted by Unknown on 5:46 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added