Simu ‘vimeo’ zamfanya Lady Jaydee kutumia namba ya Gadner
Kuna wakati unaweza kupokea simu ama kutumiwa ujumbe wa simu utakaoweza kuhatarisha ndoa/uhusiano wako na kukufanya uzichukie kabisa simu.
Kwa watu maarufu usumbufu wa aina hii ni jambo lisiloepukika. Simu kutoka shabiki anayetaka kuongea naye kwa nusu saa nzima wakati ana mambo ya kufanya ama promoter mwenye hela pungufu anayepiga simu kila baada ya nusu saa kubembembeleza show, aaah! Mbona ni vitu vya kawaida!
Kwake Lady Jaydee usumbufu huu umemchosha kiasi cha kuamua kutumia simu ya muwewe Gadner G Habash!
Maana yake ni kuwa, sasa hivi ukitaka kuongea naye lazima upitie kwenye simu ya mwenye mali (Captain G).
Hiyo imebainika baada ya mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata alipotweet kumuuliza namba anayoitumia mwanamuziki huyo wa ‘Siku Hazigandi’, “ bidada,are you using the same number?Nakutafuta.”
“Am using Gardner’s number my love, naogopa simu vimeoo but call me anytime aiiight!!!” alijibu Jaydee.
Habari ndio hiyo. Gadner yupo tayari kudeal na simu zote vimeo zisizo na kichwa wala miguu kwa Jide, so watch out you might find yourself in a big! big! Trouble.