Kigi, Mrwanda sasa rasmi Simba
WAKATI mabingwa wa soka nchini, Simba wakimalizana rasmi na wachezaji Kigi Makasi na Danny Mrwanda kwa ajili ya kuvaa jezi nyekundu msimu ujao, beki wa timu hiyo, Juma Nyoso amesema yeye ni mchezaji halali wa Wekundu hao wa Msimbazi na taarifa na kwamba mkataba wake umekwisha ni hazina ukweli.
Habari toka ndani ya klabu hiyo ambazo Mwananchi imezipata, Mrwanda na Kigi walikamilisha mipango yote jana mchana, huku Victa Costa akiachwa na Salum Machaku na Obadia Mungusa wakijiandaa kuondoka kwa mkopo.
Kigi anajiunga Simba baada ya zaidi ya misimu mitatu akiwa na klabu ya Yanga ambapo amamaliza mkataba wake.
Nyoso alisema hayo muda mfupi baada ya kurejea nchini jana akitoka Ivory Coast alikokwenda na Stars kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi kucheza fainali za Kombe la Dunia na kufungwa mabao 2-0.

Alisema anachofahamu ni kwamba, mkataba wake wa miaka miwili na Simba unamalizika Desemba mwaka huu.
Kauli ya Nyoso imekuja baada ya siku kadhaa za uvumi kwamba yeye ni miongoni mwa wachezaji wanaojiandaa 'kurushiwa' virago msimu huu wakiwamo pia Juma Jabu, Uhuru Selemani na Gervais Kago.
Kauli ya Nyoso imekuja baada ya siku kadhaa za uvumi kwamba yeye ni miongoni mwa wachezaji wanaojiandaa 'kurushiwa' virago msimu huu wakiwamo pia Juma Jabu, Uhuru Selemani na Gervais Kago.
Jana, Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage alipoulizwa mkataba wa Nyoso na suala zima la usajili, alisema anatarajia leo kutoa taarifa yenye majibu suala hilo na mengine kuhusu wachezaji wanaoachwa na wanaosajiliwa.
Akiongea na Mwananchi jana, Nyoso alisema binafsi hajaongea lolote na viongozi wake, na kwamba taarifa za kuachwa kwake anazisikia na kuzisoma kwenye vyombo vya habari.
Akiongea na Mwananchi jana, Nyoso alisema binafsi hajaongea lolote na viongozi wake, na kwamba taarifa za kuachwa kwake anazisikia na kuzisoma kwenye vyombo vya habari.
"Simba tunafuata kanuni na sheria za usajili, hatuongea kinyume na mambo hayo, sasa leo nitatoa ufafanuzi wa kila jambo kuhusu usajili," alisema Rage.
"Nimemaliza mkataba Simba, nani kasema? Sifahamu lililotokea nyuma kwani ndiyo kwanza nafika. Nalofahamu mimi ni kwamba, nina mkataba na Simba bado," alisema Nyoso.
Nyoso, alisema anachofahamu yeye ni kuwa atabaki Simba mpaka mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa mwaka huu na siyo kinyume chake.
"Siwezi kuzungumzia mikakati yangu kwa sasa, nadhani ni mapema zaidi hasa ukizingatia ndiyo kwanza nimerudi na timu ya taifa, ila baada ya siku mbili naweza kuongea jambo," alisema Nyoso.
Nyoso aliyejiunga na Simba toka Ashanti iliyowahi kucheza Ligi Kuu kabla ya kushuka daraja, alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Msimbazi.
Beki huyo ambaye amecheza mechi zote za Ligi Kuu zilizoipa ubingwa wa Bara Simba, anadaiwa kuwa mtovu wa nidhamu ndiyo maana klabu yake imepanga kuachana naye.
Nyoso pia alikuwa na mchango mkubwa ulioifikisha Simba hatua ya 16-bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho kabla ya kuondolewa kwa mikwaju ya penalti na timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
Aidha Mwananchi ilipomtafuta Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Rage alisema wao wanafuata sheria na kanuni za usajili hivyo leo wanataraji kutolea ufafanuzi masuala yote yahusuyo usajili wa wachezaji wao wote.