Zanzibar Kimenuka..Angalia tukio katika picha
Baada ya jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wafuasi wa kikundi cha uamsho kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa kiongozi wao, hali inaendelea kuwa tete na hivi sasa baadhi ya wafuasi hao wameingia mtaani wakishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo huku jeshi la polisi likilazimika kutumia mabomu kuwatawanya wafuasi hao …..Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini.
Waanamanaji hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja vya Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani Maskani ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya Lumumba.
Maandamano hayo walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa lililoandaliwa na Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la kuzungumzia mfumo wa elimu Zanzibar.
Akizungumza na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao ndani ya nchi yao....................
“Sisi wazanzibari kama wananchi wengine wowote duniani tuna haki ya kikatiba kudai nchi yetu kama walivyodai Sudan ya Kusini, mbona Sudan ya wameweza kujitenda na kupata nchi yao kwa nini sisi kama wazanzibari tusikubaliwe kudai nchi yetu sasa sisi tunampelekea salam katibu mkuu wa umoja wa mataifa kumwambia kuwa wazanzibari sasa wanataka nchi yao” alisisitiza Sheikh Farid huku akiungwa mkono kwa mamia hao kuinua mikono na kusema ndiooooo.
Katika
 kuonesha kwamba hawataki  tume ya katiba ije kuchukua ya maoni ya 
katiba mpya Sheikh Farid alisema  wanataka kwanza kuamuliwe suala la 
Muungano kabla ya jambo lolote na  kuahidi kwamba wataendelea kufanya 
makongamano, mihadhara na maandamano  kwa kadiri wawezavyo hadi hapo 
serikali itakaposikia kilio hicho.
“Ujumbe
 huu tunautoa kwa Ban Kin  moon, na kwa ulimwengu mzima lakini pia 
tunataka rais wetu Dk Shein  asikie kilio hiki na Rais Kikwete ambaye 
yeye ni mtetezi wa haki za  binaadamu na pia ni mfuatiliaji wa nchi 
zinazovunja haki za binaadamu  tunataka asikie kilio cha wazanzibari 
kuwa wanataka nchi yao” alisema.
Alisema
 juzi wamefanya maombi  maalumu ya kumuombea Rais wa Zanzibar lengo 
likiwa ni kumjaaliwa kheri  na awe na maamuzi sahihi juu ya wananchi wa 
Zanzibar sambamba na  kuwaomba Makamu wa Kwanza na makamu wa Pili wa 
Zanzibar kusikia kilio  cha wazanzibari wasiotaka Muungano.
“Tunamuomba
 Rais wetu Dk Shein,  Makamu wa Kwanza Maalim Seif na Makamu wa Pili 
Balozi Seif kwamba sisi  wazanzibari tunahitaji Zanzibar huru, 
tunahitaji heshima ya nchi yetu na  tupo tayari kwa lolote kwa hivyo 
tunataka salamu hizi na ujumbe huu  ukufikieni” alisema Sheikh Farid 
huku akiungwa mkono na maelfu  waliohudhuria katika kongamano hilo 
ambalo awali liliandaliwa kwa lengo  la kuzungumzia masuala la elimu na 
mfumo wake.
Akiendelea
 kutoa salamu hizo  mara Sheikh Farid alisoma kifungu cha 16 cha katiba 
na kuwaleza wananchi  kwamba haki ya kutembea ni haki ya kila mwananchi 
ambayo imeainishwa  katika katiba na sheria za haki za binaadamu hivyo 
aliwageukiwa na  kuwataka wasimame na kisha kumfuata yeye.
“Haki
 ya kutembea ni haki ya  msingi kwa mujibu wa sheria na kifungu cha 16 
kinatupa haki ya kutembea  sasa mimi nataka kutembea jeee mpo tayari 
kutembea na mimi? Alihoji  Sheikh huyo huku akijibiwa na umma mkubwa 
kwamba ndioooo”
Aliongeza
 kwamba “Tunaanza  kutembea na tuone mtu atukamate tunakwenda njia ya 
kinazini, tunapita  michenzani, tunapita barabara ya kwa biziredi na 
kisha tunarejea hapa  hapa kuendelea na kongamano letu kwa amani kabisa 
mmesikia….akajibiwa  ndiooooo”
baada
 ya kusema hivyo Sheikh  Farid alitoa takbir na kuanza kukamatana mikono
 na viongozi wenzake na  huku ummati mkubwa ukiwa umekamatana mikono 
nyuma na kuanza safari kwa  pamoja na kutembea katika barabara ambazo 
walizitaja awali.
Waandamani
 hao walikamata  mabango yenye maandishi mbali mbali ikiwemo hatutaki 
muungano, tunataka  nchi yetu, zanzibar bila ya muungano inawezekana na 
wengine kadhalika  huku wakitembea njiani na kupiga takbir ambapo 
walikuwa wakisema  Mwenyeenzi Mungu Mkubwa, Mwenyeenzi Mungu Mkubwa sisi
 hatuna uwezo  isipokuwa tunakutegemea wewe Mwenyeenzi Mungu.
Waandamanaji
 hao walianza  kutembea kwa utaratibu maalumu huku magari yakisimama na 
kuwapisha bila  ya kuwepo jeshi la polisi ambapo viongozi wa jumuiya 
hiyo na wananchi  wengine waliongoza utaratibu huo na kutembea katika 
barabara kwa  utaratibu mzuri hadi kumaliza maandamano yao waliyoyaita 
matembezi ya  amani.
Baadae
 jeshi la polisi lilifika  katika eneo ambalo kumefanyika maandamano 
hayo na kufungua mabango yao  ya kuwataka watu kuondoka lakini wakati 
magari hayo ya polisi matatu  yanafika eneo hilo la Kariakoo tayari 
ummati mkubwa ulikuwa umeshapita  katika eneo hilo na hivyo kuingia 
ndani ya magari yao na kuondoka kwa  salama.
Awali
 akitoa mada katika  kongamano hilo, Maalim Abdulhafidh Malelemba 
alisema sekta ya elimu  imekuw aikidorora Zanzibar kutokana na 
kukandamizwa na mambo ya Muungano  ambapo kila mwaka wanafunzi 
wanapofanya mitihani kufelishwa kwa  makusudi huku idadi ya wanafunzi 
wanaokwenda katika vyuo vikuu wakiwa  kidogo kutokana na kufelishwa 
katika mitihani ambapo husainiwa na baraza  la mithani Tanzania (NECTA).
Wakizungumza
 katika nyakati  tofauti katika kongamano hilo, baadhi ya walimu 
walisema kukosekana kwa  baraza la mitihani Zanzibar kusimamia mitihani 
ya elimu ya juu ndio  sababu ya wazanzibari kufelishwa kwa wingi na 
kushindwa kuingia katika  vyuo vikuu kwa kuwa wanafunzi wengi wa 
Zanzibar hufelishwa.
Walimu
 hao walitoa ushahidi wa  hivi karibuni wa kufelishwa wanafunzi wa 
kidatu cha nne ambapo walisema  lile ni tukio la makusudia lililofanywa 
na baraza la mitihani ikiwa ni  kuwadhoofishwa wanafunzi wa Zanzibar ili
 wasiendelee katika masomo kwa  kuwafelisha.
Habari kwa hisani ya www.zanzibaryetu.wordpress.com





