Sababu Halisi ya Chris Brown Kumdiss Rihanna Yagundulika
Imebainika
kuwa Chris Brown alikuwa anataka kurudiana na Rihanna huku akiendelea
na uhusiano na mpenzi wake wa sasa Karrueche Tran, kitu ambacho Rihanna
alikikataa.
Licha
ya wasanii hao kushirikishana kwenye remix za nyimbo zao mapema mwezi
uliopita, mambo yaligeuka tena baada Chris kudaiwa kumtukana Rihanna
kwenye wimbo.
Chris alipenda warudiane na Rihanna lakini wakati huo huo alikataa kumwacha Karrueche.
Hatimaye
Rihanna alimwambia Chris Brown kuwa anataka kuanzisha uhusiano na mtu
mwingine kama (Chris) hatoweza kuchagua kusuka ama kunyoa.
“Chris
hakuwa tayari kuukatiza uhusiano wake na Karrueche, japokuwa alimfanya
Rihanna aaminini kuwa alikuwa bado akimpenda sana,” chanzo kimoja
kimeuambia mtandao wa Hollywood Life.
“Chris
ndiye aliyekuwa wa kwanza kumfuata Rihanna na kumuomba msamaha.
Alionesha mahaba mazito kwake wakati akimbembeleza na kumwambia namna
alivyommiss, jinsi asivyoweza kumfananisha Karrueche na yeye na namna
anavyotaka kusawazisha mambo.”
Chanzo
hicho kiliendelea kusema “Chris wanted to have his cake and eat it
too!” Once Rihanna made it clear that she wouldn’t stand to be his side
chick, Chris dissed her.”