Exclusive Audio: Capital FM ilipowahoji Jaguar na Prezzo!
Wiki hii Prezzo ameachia ngoma iitwayo The Greatest ambayo amemdiss Jaguar kitu kinachoashiria kuwa beef hii haijaisha.
Tungependa kukupa nafasi ya kusikiliza interview walizowahi kufanyiwa na Capital Fm kuhusiana na beef yao.
Katika interview ya Jaguar na radio hiyo maarufu nchini Kenya Jaguar aliongea mengi ya kumponda Prezzo.
Alizungumza kuwa anamshangaa Prezzo kujidai kuwa anavyaa bling bling wakati akipanda kwenye stage watu wanamzomea.
Jaguar aliendelea kujinadi kuwa yeye sasa hivi ananunua ardhi wakati Prezzo anauza na kuwa hizo Gucci ambazo Prezzo hujisikia kwenye nyimbo ni fake ama za mtumba na anajua wapi huzinunulia na kuongeza kuwa rais huyo wa CMB yuko broke kiasi cha kushindwa kuwanunulia hata pombe washkaji.
Jaguar alisema pia kuwa yeye hutoa mkopo wa fedha hivyo kama Prezzo akihitaji anamkaribisha.
Msikilize Jaguar zaidi hapa:
Kwa upande wa Prezzo alipopigiwa kuzungumzia suala hilo alisema tu kuwa hamjui kabisa Jaguar zaidi ya kujua aina ya gari yenye jina hilo.
Msikilize alivyozungumza hapa!