Ay na Producer wake mpya Marco Chali wawasili Johannesburg kushoot video
Rapper, mwanamuziki na mjasiriamali wa Tanzania Ambwene Yesaya akiwa na producer Marco Chali wa Mj Records leo asubuhi wamewasili mjini Johannesburg nchini Afrika kusini kushoot wimbo wa msanii huyo.
Katika mtandao wa twitter AY ameandika “In Johannesburg wit @Marcochali..Cool weather..ready 2 shoot my new video with @I_Am_Godfather cc @ArthurSamTz@Murunga_Josh”
Video hiyo ambayo imedaiwa itagharimu dola za marekani 20,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 31 za kitanzania itafanywa na kampuni iitwayo Godfather Productions ya Afrika kusini inayomilikuwa na Micheal Uche Ogoke.
Kwa mujibu wa Ogeke aka Godfather, shooting ya video hiyo itafanyika alhamis hii mjini Johannesburg.
Kampuni hiyo imeshafanya video za P Square na Flavour wa Nigeria na wiki hii ina ratiba ya kufanya video nyingine ya kundi la P-Square mjini Johannesburg na Capetown.