Chris Brown Auza Nyumba Yake Baada ya Majirani Kumchoka
Tangu ahamie mwaka jana kwenye nyumba yake ya huko West Hollywood, Los Angeles, California, Chris Brown amekuwa akigombana kila siku na majirani zake. Ndio maana si jambo la kushangaza kuamua kuiuza nyumba yake yenye vyumba vitatu kwa gharama ya $1.895million – ikiwa ni zaidi ya $300,000 ya bei aliyoinunulia yeye February 2011. Kila anapokuja kuishi kwa muda katika nyumba hiyo iliyopo kwenye eneo la square 3,000 majirani wamekuwa wakimlalamikia kwa kufungulia muziki kwa sauti ya juu hasa usiku na mbwa kubweka usiku kucha. Baada ya shutuma nyingi kuhusu tabia zake katika eneo analoishi kuandikwa na mtandao wa TMZ, aliandika kwenye Twitter mwaka jana ‘A person should be able to live in his or her own company of their house! I’m barely home so these stories and accusations are so childish! My neighbour also calls the parking enforcement everyday so I get a 360 dollar ticket for each of my cars. (everyday).’ Chris mwenye miaka 22 huwa hakai sana kwenye mjengo wake kwakuwa muda mwingi anakuwa barabarani kupiga show. Nyumba hiyo pia ina mabafu manne, eneo kubwa la jiko, ofisi na kila chumba kinajitegemea kwa kila kitu. Kutokana na malumbano ya kila siku na majirani, Chris alihama West Hollywood na hivi karibuni amenunu nyumba nyingine yenye thamani ya $1.5million huko Hollywood ambayo ina swimming pool. Souce: