Rapper wa Tanzania Alishwa Madawa na Kuibiwa Kila Kitu!
Rapper Janb Kiwia aishie nchini Sweden amesema jana amelishwa madawa na kisha kuibiwa kila kitu alichokuwa nacho baada ya kualikwa kwenye club moja ya mjini Stockholm kutambulisha nyimbo zake.
Kupitia Facebook msanii huyo ambaye yupo kimasomo nchini Sweden amesema “You drug me and took my new iPhone & etc !!! shit, trust me i will find you ni***. Friends poor me, my iPhone & everything is gone! Damn!
Ameendelea kwa kusema “Vijana wamechukua mali zao banaaa ila ntawapata tuu maake simu yangu iko registered na apple labda waitumie kama toy, mali nyingine hizo wameshinda na wamechukua…Dah!! Always careful ila haujui kulishwa madawa usiombe ikakutokea, na ndo imenitokea kwa mara ya kwanza. wameniliza kila kituuuuu machalii”
Wakati marafiki na watu wake wa karibu wakiendelea kumpa pole kwa yaliyomkuta Janb ameendelea, “I feel sorry for myself and him, this ni*** took stuffs from a poor guy who is hustling every day!!?”
Janb amesema watu hao walimwekea madawa kwenye bia na hakumbuki ilikuaje lakini tayari amemfahamu mtu aliyemuibia vitu vyake.