ALBAM YA WEUSI YAKWAMA


Staa wa hip hop kutoka 'Kruu' ya Weusi iliyokita kambi  pande za A-Town, Nikki wa Pilli amesema kuwa albam ya kundi hilo iliyokuwa itoke mapema mwezi uliopia imekwama.
Akizungumza na teentz.com mapema leo Nikki anayepewa heshima ya kuwa mmoja wa mastaa wa muziki huo wenye uwezo wa kuandika mistari mikali alifunguka kuwa kukwama kwa albamu hiyo kumekuja kufuatia matatizo ya kiufundi baada ya waliokuwa wakisimia kukamilika kwake kushindwa kuambatanisha moja ya wimbo katika  uliokuwa ndani ya albam hiyo baada ya kufutika kutoka katika kumbukumbu za komputa.
"Ni jambo ambalo limetusikitisha hata sisi kwa kuwa tulikuwa tunajuwa kuwa mashabiki wetu wanahitaji albam hiyo, wimbo mmoja umefutika ndiyo sababu kubwa ya kukwama kutoka lakini hata hivyo fans wetu wasiwe na wasi wasi kwani tayari tatizo hilo limeshughulikiwa na soon tutawatangazia  tarehe ya kutoka tena  kwa mzigo huo" alisema  Nikki.

1:27 AM | Posted in | Read More »

STAA BONGO MOVE APIGWA STOP KUIGIZANyota  kutoka tasnia ya  filamu Bongo Skyner Ally huenda asionekane tena kwenye ulimwengu wa move kufuatia kupigwa  stop kushiriki katika  kuigiza.

Stori  'under carpet' ambazo Teentz.com imezinyaka kutoka kwa mmoja wa wapambe wa mwigizaji huyo aliyeng'arisha nyota yake kupitia filamu ya  'SECOND WIFE' iliyopikwa na mkali Ray Kigosi, zinasomeka kuwa  Skyner amepigwa stop na  wazazi wa  upande pili  (wakwe) ili aweze kulea vizuri mtoto wake badala ya kutumia muda mwingi akiwa kambini na waigizaji wengine kwa ajiri ya kurekodi 'muvi'.

"amezuiwa, na sijui kama ataruhusiwa kipindi cha  karibuni  na  huenda  ikawa moja kwa moja  kwani ameambiwa atulie alee familia na mtoto wake, alisema mpambo huyo.

"kuona hivyo, Teentz ilimvutia waya  msanii  huyo na  majibu yake yakawa  hivi: unaweza kuona nimezuiwa lakini kwangu mimi sijachukulia hivyo kilichopo ni kuwa  nimetulia kwanza nilee mtoto wangu na familia pia, kwa sasa nipo Tanga nimekuja kusalimia ndugu na baada ya muda nitarejea Dar halafu ndiyo nitatoa jibu kamili kama  nitaendelea ama la" alisema Skyner.


1:24 AM | Posted in , | Read More »

CHEGE APATA AJALI, AJERUHIWAMsanii wa Kigoma All Stars Chege Chigunda usiku wa jana amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zimesema kuwa usiku huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi kwa shughuli kadhaa za kimuziki.

Katika mahojiano ya dakika chache na mtangazaji wa Clouds FM, Diva kwenye kipindi cha Ala za Roho, Chege amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana pikipiki katika mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata ajali hiyo , Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele.…

1:21 AM | Posted in , | Read More »

Mario Van Peebles kuzindua filamu yake Mlimani City


Wakazi wa Dar es Salaam watanufaika na ujio wa muigizaji na muongozaji wa filamu wa Hollywood Mario Van Peebles aliyealikwa mwaka huu kama mgeni wa heshima kwenye tamasha la filamu la kimataifa Zanzibar, ZIFF.
Van Peebles ataizindua filamu yake ya mwaka huu iitwayo ‘We The Party’ ambayo ameiongoza na kuigiza pia.
Kwa ushirikiano na ZIFF, kutafanyika ‘red carpet premier’ ya filamu ya ‘We the Party’ kwenye ukumbi wa Century Cinemax cinema wa Mlimani City.
Tukio hilo litahudhuriwa na yeye mwenyewe Mario Van Peebles na mwanae wa kiume Mandela Van Peebles aliyeigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu hiyo.
Filamu hiyo itaoneshwa kwa siku tano mfululizo ili kutoa muda zaidi kwa watu kuiona.
We The Party iliyoigizwa jijini Los Angeles inahusisha marafiki watano wanafunzi wa high school wanaozungukwa na mapenzi, pesa, kujirusha, chuo, sex, bullies, Facebook na mambo mengine.
Rapper Snoop Dogg anaye ameigiza kwenye filamu hiyo

9:55 PM | Posted in , | Read More »

Polisi atishia kumuua Michelle Obama


Afisa wa polisi wa jijini Washington D.C. anayehusika na kulinda maafisa wa ikulu ya White House nchini Marekani, amejikuta akipumzishwa kazi baada ya kudaiwa kutishia maisha ya First Lady, Michelle Obama.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, ofisa huyo anafanya kazi ya escort ya pikipiki na anadaiwa kusema kuwa angempiga risasi First Lady huyo.
Inasemekana aliwaonesha polisi wenzake picha ya bunduki ambayo angeitumia kumuulia.
Hata hivyo idara ya polisi ya jijini Washington imesema haina maelezo mengi kuhusiana na tukio lakini msemaji wake Gwendolyn Crump amesema kwenye maelezo:
“We received an allegation that inappropriate comments were made. We are currently investigating the nature of those comments.”
Idara hiyo pia iliwasiliana na ‘Secret Service’ kuhusiana na kitisho hicho.
Msemaji wa Secret Service Ed Donovan amesema mamlaka hiyo inalifahamu tukio hilo na inachukua hatua zinazotakiwa kwa uchunguzi maalum.

9:53 PM | Posted in , | Read More »

Mama yao Psquare alifariki baada ya upasuaji wa moyo


Sababu ya kifo cha Josephine Okoye,mama wa nyota wa muziki wa R & B nchini Nigeria wa kundi la Psquare, Peter na Paul imejulikana.
Maelezo ya msemaji wa Psquare yamesema mama yao alifariki saa chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo nchini India.
Mrs.Okoye alipelekwa nchini India kwaajili ya kufanyiwa operation baada ya kukaa katika hospitali ya St.Nicholas ya nchini Nigeria kwa muda, ambayo ni miongoni mwa hospitali ghali nchini humo.
Wakati huo huo, watu maarufu wamekuwa wakimimika kwenye nyumba ya kifahari ya P-Square iitwayo Square Ville, kuungana na ndugu na jamaa kwenye msiba huo.
Mastaa wengi wametumia mtandao wa Twitter kuwapa pole wasanii hao kwa kumpoteza mama yao.
Rita Dominic ‏@ritaUdominic
My heart goes out to the Okoye family today. RIP Mrs. J. Okoye God be with you!
D’banj kokomaster ‏@iamdbanj
My sincere condolences go out to Peter, Paul and the entire Okoye family. May the Lord be a comfort and strength to you at this sad time.
Pamoja na watoto wanne aliokuwa nao, Mrs Okoye ameacha mjukuu mmoja kutoka kwa Peter Okoye aliyezaa na Lola Omotayo.

9:51 PM | Posted in , | Read More »

Simba Wafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki


Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki jana.
Na Wilbert Molandi
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba, jana walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki baada ya kuifunga Azam kwa penalti 3-1, kufuatia dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao ya Simba ndani ya dakika 90 yalifungwa na Felix Sunzu katika dakika ya 29 na Mwinyi Kazimoto aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90, wakati yale ya Azam yalifungwa na Hamis Mcha (45) na John Bocco (81)
Katika mikwaju ya penalti, Mwinyi Kazimoto, Amir Maftah na Kigi Makasi ndiyo walioifungia Simba wakati Haruna Moshi ‘Boban’ alikosa, wakati Azam ikipata penalti yake kupitia kwa Mcha huku Haji Nuhu, Himid Mao na Ibrahim Mwaipopo wakikosa.
Wakati ikionekana kuwa Simba wangekwenda mapumziko wakiwa wanaongoza, Azam walifanya shambulizi la kushtukiza na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 45 baada ya Tchetche kumpigia krosi Hamis Mcha aliyeifungia Azam bao la kusawazisha.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ni Azam ndiyo iliyotangulia kujipatia bao lakini Simba wakasawazisha.
Mara baada ya mchezo huo Kocha wa yanga Tom Saintfiet ambaye alishuhudia mchezo huo uwanjani hapo akiwa jukwaani kwa mashabiki wa Yanga alisema Simna ni timu nzuri na imecheza vizuri, pia alimsifia Sunzu kwa kusema kuwa anatakiwa kuchungwa kwa kuwa anaonyesha ana madhara makubwa.
Kocha wa Simba, Milovan Circovic alisema hajaridhishwa na uimara wa wachezaji wake licha ya kuibuka na ushindi huo, hali ambayo inaleta hofu katika ushiriki wao wa michuano ya Kagame inayoanza kesho. Wachezaji ambao anadai hawakuwa imara ni Boban, Kazimoto na Juma Nyosso.
Kocha Msaidizi wa Azam, Kally Ongala alilalamikia bao la pili la Simba kwa kudai kuwa mshambuliaji Danny Mrwanda alijiangusha eneo la hatari, hivyo hawakustahili kupata penalti iliyozaa bao la kusawazisha kwa wapinzani wao.

9:50 PM | Posted in , , , | Read More »

Wema Sepetu Avamiwa na majambazi


Na Musa Mateja
SIKU chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa huku gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.
KIKWAZO CHA NGUVU
Hata hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti, majambazi hayo yalishindwa kuingia ndani kabisa kutokana na milango madhubuti iliyopo kwenye nyumba hiyo ya kisasa.
WAJIPOZA KIDOGO
Kule ndani ya geti, walivunja mlango wa gari hilo na kuiba vitu mbalimbali kama kifaa cha kudhibiti mwenendo wa umeme ndani ya gari (control box), vifaa vya kufungulia vioo, milango na madirisha (power window) na vioo vinavyomuongoza dereva kuona nyuma (side miller).
Vitu vingine ambavyo viliambatana na wizi huo ni ‘makapeti’ ya ndani na vitu vingine vidogovidogo ambavyo vilikuwa ndani ya geti hilo.
WEMA AWASHANGAA WALINZI WAKE
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Wema alisema kuwa hata yeye ameshangazwa na uvamizi huo ambao umemfanya kuibua maswali mengi kuliko majibu hasa akizingatia kuwa tukio hilo limetokea wakati nyumba yake ina walinzi wawili.
“Ni kweli nimeibiwa hivyo vitu kwenye gari na vingine vilikuwa nje, ila mazingira ya kuvamiwa na yale majambazi yananitia shaka sana maana walinzi wangu wawili walikuwepo muda wote, sasa sijui nini kilitokea?” alisema Wema kwa sauti ya kupooza.
Akaendelea: “Sikuwa na namna kwao, nilikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ili angalau nisaidiwe utatuzi wa jambo hili sambamba na kuwabananisha walinzi wangu ambao walikuwepo usiku wa tukio.
“Naamini kama geti la kutokea nje lingekuwa legelege, wangeiba na gari lenyewe. Lakini hili geti ni gumu, mpaka kulifanya lifunguke wangeweza kuchukua masaa matano ambapo kungekuwa kumekucha.”
INAWEZEKANA SABABU IKAWA HII?
Katikati ya Juni mwaka huu, staa huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, alitangaza kupitia runinga kwamba anamiliki nyumba hiyo huku akisema ina kila kitu ndani.
Kwa mujibu wa picha zilizoenea kwenye mitandao mbalimbali Bongo, sebule ya nyumba hiyo inaweza kushawishi ‘wazee wa kazi’ kunyatia kwani Meneja wa Wema, Martin Kadinda alisema manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na samani zake shilingi Milioni 4OO ‘ziliteketea’.
HABARI ZA KIPOLISI ZATHIBITISHA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Charles Kenyera hakupatikana siku ya Jumanne kuzungumzia tukio hilo licha ya kwamba, habari za kipolisi zilithibitisha Wema kukumbwa na uvamizi wa watu wanaodhaniwa ni majambazi.

9:47 PM | Posted in , , | Read More »

Fani Ya Umodo na Ushoga


.FANI ya u-modo (mitindo) ambayo awali ilionekana kuwa nyuma nchini Tanzania, sasa imeshika kasi baada ya akina dada warembo na wakaka watanashati kujikita huko.
Ma-miss Tanzania, Jokate Mwegelo, Victoria Martin, Nasreen Karim, Miriam Odemba, Happiness Magese na Fideline Iranga, ni miongoni mwa mifano mikubwa ambapo sasa wameamua kujidhatiti kwenye fani hiyo ili kuikuza hapa Bongo.
Kwa upande wa wanaume, Kenedy Victor ‘Kenny’, Mister University 2001, Matukio Chuma, Martin Kadinda, Ahmed Mwinyigumba ‘Mwinyi’ na Ally Remtulah (pia mbunifu wa mavazi) ni vijana wa Bongo walioegemea fani hiyo.
Mdogo wa mwanamitindo aliyepiga kambi Afrika Kusini, Dayana Nells, Wancy Nells (pichani) naye ametumbukia kwenye shughuli hiyo akifanya kazi zake na Kampuni ya Mitindonite Afrika yenye makazi yake Bongo na nje ya nchi.
Mwenyewe anasema: “Kwa kweli Bongo kwa sasa tuko juu, uanamitindo umefika mahali pa kuwa ajira si kama zamani. Nawapongeza wote wanaotupa sapoti hasa Global Publishers. Nawasihi vijana wa kiume kama mimi wajitokeze kwa wingi kwani kwenye mitindo hakuna ushoga kama baadhi ya watu wanavyovumisha.”
Wancy alitoa ushauri kwa wanamitindo kuunda chama imara kwa ajili ya kutetea maslahi yao ambapo alidai kwa sasa wengi, ukiacha wakongwe, hawajitambui.

9:45 PM | Posted in | Read More »

Aibu tupu Miss Apanda Jukwaani Bila Kufuli


Ni aibu tupu! Mnyange aliyeibuka mshindi wa pili kwenye kipute cha Miss Vyuo Vikuu au Miss Higher Learning 2012/13, Fatma Ramadhan (pichani), ameacha gumzo baada ya kukwea jukwaani akiwa kaacha wazi mlango wake wa ‘ikulu’ bila kufuli, Risasi Jumamosi linairusha hewani.
NI MBELE YA MBUNGE
Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na mwandishi wetu, lilijiri usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu kwenye Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Kisesa kwa leseni ya CCM, Mhe. Luhaga Joelson Mpina.
Katika tukio hilo ambalo hata mheshimiwa mbunge aliliona na kutazama pembeni, ilifahamika kuwa mrembo huyo aliyetimba jukwaani akiwa hajavaa nguo ya ndani, alitokea kwenye Chuo Cha Uandishi wa Habari mkoani Arusha.
“Jamani… jamani! Yaani huyu binti yuko uchi kabisa, imekuwaje au kajisahau? Ni aibu iliyoje, tena mbele ya mheshimiwa mbunge? Hii kweli aibu tupu,” alisikika mmoja wa watazamaji wa kinyang’anyiro hicho.
RASHIDA NAYE AANIKA MAMBO
Katika tukio lingine la aibu kwenye ‘iventi’ hiyo, kivazi cha mkufunzi wa warembo ambaye ni Miss Mara 2000, Rashida Wanjara kiliacha watu midomo wazi baada ya kuanika mambo yake nyeti ya mwilini.
“Duh! Huyu naye kiboko. Yaani kila kitu mpaka vya chumbani kaviacha hadharani?”
HEBU MSIKIE
Risasi Jumamosi lilipomvaa na kumuuliza kulikoni kuvaa kigauni kinachoonesha maungo yake nyeti, alifunguka: “Mimi ndiye miss nisiyechuja, nikiamua kushiriki umiss bado nakubalika na mwili wangu unalipa.”

9:43 PM | Posted in , | Read More »

Vita kati ya imani ya Freemason na makanisa


SASA ni vita! Si vingine ni kati ya imani ya Freemason na makanisa. Mchungaji wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (E.A.G.T) lililopo Kipunguni B, Dar, Julius Mwamkamba amevujisha siri ya kushawishiwa na Freemason ajiunge nao kwa makubaliano ya kumjengea kanisa la kisasa, Risasi Jumamosi linatiririka nayo.
MCHEZO ULIVYOANZA
Akizungumza na mapaparazi wetu juzikati, jijini Dar, Mchungaji Mwamkamba alisema awali alitoa matangazo na pia kutuma ujumbe mfupi wa simu ‘SMS’ kwa watu mbalimbali akiomba mchango wa fedha ili aweze kujenga kanisa lake, lakini bila matarajio yake, namba zake ziliangukia mikononi mwa watu hao.
“Nilitarajia kupanua kanisa langu hivyo nilihitaji mchango wa fedha kwa ajili ya ujenzi, nikatoa tangazo kwa watu mbalimbali pamoja na kutuma SMS kwa marafiki zangu.
“Siku moja nilipigiwa simu na watu nisiowajua, wakaniambia wanataka kukutana na mimi ili wanisaidie fedha  za ujenzi wa kanisa langu.
“Nilikubali, nikaenda kukutana nao pale Ubungo. Walianza kunieleza jinsi walivyoamua kunisaidia kujenga hekalu la Mungu huku wakisema wananipa fedha za kutosha na kuagana na umaskini,” alisema Mchungaji Mwamkamba.
Aliendelea kudai kuwa watu hao walisema lengo lao ni kumpa kiasi chochote cha fedha ambacho kilikuwemo kwenye ‘brifkesi’ kwa ajili ya ujenzi huo.
“Waniliambia wananipa kiasi chochote cha fedha ninachokihitaji, lakini iwe siri yangu na wao, halafu wakasema waumini katika kanisa langu wataongezeka.

MCHUNGAJI AZIDI KUFICHUA
“Wakaniambia wamefanya hivyo kwa watumishi wengi wa Mungu hapa Tanzania ambao kwa macho ya kawaida huwatambuliki kama ni wafuasi wa Freemason na wanafanya ishara na miujiza mingi huku makanisa yao yakiwa na idadi kubwa ya waumini.”

APEWA MKATABA
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na kabla mchungaji huyo hajasema ndiyo au hapana, alipewa mkataba wenye maelekezo ya jinsi ya kujiunga ili aanze kula mema ya nchi na kuuaga umaskini kwa muda mfupi.
“Walinipa mkataba, una nembo ya Freemason, lakini wakaniambia ni lazima nibadili dini, nianze kuvaa nembo ya mwewe na nyoka na kumtoa kafara mke wangu au mwanangu nimpendaye kama sadaka ya shukrani kwa mungu wao,” alisema mchungaji.

AWACHOMOLEA WAZI
“Niliposikia masharti hayo, ghafla nilisikia uchungu moyoni, nikakataa, nilisimama haraka sana na kuondoka kwa mwendo wa haraka, kama nakimbia. Wakaanza kunizomea huku wakitoa ishara ya kuvunja vidole viwili ambayo ni moja ya alama za Freemason,” alisema mchungaji huyo.

KWA NINI NI VITA?
Hivi karibuni, Mchungaji wa Kanisa la Good News for All Nations, Mark Diganyeka alitoa alama za kuwatambua watumishi wa Mungu ambao ni waumini wa dini ya Freemason na kusema kuwa waumini wawe makini kuwabaini.
Miongoni mwa alama hizo alisema ni pamoja na kuvunja vidole kwa haraka wakati wakihubiri na kuvaa pete kubwa kwa ajili ya kufanyia miujiza wawapo madhabahuni.
Kwa tafsiri ya Mchungaji Diganyeka na hayo aliyokutana nayo Mchungaji Mwamkamba, ni dhahiri  makanisa yameingiliwa na Freemason hivyo kuanza kutimia kwa yale maneno kwamba, imani hiyo itawavaa watumishi wa Mungu kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo.

9:41 PM | Posted in , | Read More »

SAJUKI SHAVU... DODO


AFYA ya staa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ imetengemaa ambapo sasa shavu dodo baada ya kupata matibabu ya kutosha nchini India alikokwenda kutibiwa hivi karibuni, Amani limemshuhudia.
Jumatatu wiki hii, timu ya waandishi wa Global Publishers ilipiga hodi nyumbani kwa Sajuki na mkewe, Wastara Juma, Tabata-Bima jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumjulia hali.
WASOMAJI WATAKA KUJUA HALI YA SAJUKI
Awali, baadhi ya wasomaji wa magazeti ya Global walikuwa wakipiga simu mara kwa mara kwenye chumba cha habari wakitaka kujua maendeleo ya staa huyo anayesumbuliwa na uvimbe tumboni.
Hapa tunamnukuu mmoja wa wasomaji wetu: “Jamani mmekuwa mkituandikia habari za afya ya Sajuki, tangu kuanza kuumwa, kuzidiwa, kupelekwa India na aliporudi, lakini kipindi kirefu kimepita mmekuwa kimya, vipi jamaa anaendeleaje kwani?”
MAPAPARAZI WAFUNGA SAFARI
Kufuatia sitofahamu hiyo ya wasomaji, Jumatatu ya wiki hii waandishi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwa wawili hao.
WASTARA AKENUA MENO
Tofauti na siku za nyuma, safari hii Wastara alipowaona mapaparazi wakiingia kwake alionesha meno yote huku akiwakaribisha kwa ukarimu wa hali ya juu.
Msikilize mwenyewe: “Jamani, karibuni sana, yaani mmekuja kutujulia hali? Mungu awaongezee kwa kweli. Karibuni ndani, piteni tu, hakuna haja ya kuvua viatu.”
SAJUKI AJAA TELE KWENYE KOCHI
Tofauti na siku za nyuma alipokuwa amezidiwa, siku hiyo Sajuki alikutwa amekaa kwenye kochi akiwa amevaa ‘traksuti’ na alipowaona waandishi na yeye alitabasamu huku akisema:
“Ohooo! Karibuni sana, karibuni ndani, piteni.”
Bila kupoteza muda, Sajuki aliwaambia waandishi afya yake inavyoendelea huku akisisitiza kwamba anamshukuru sana Mungu.
“Kwa kweli jamani bila kuficha namshukuru sana Mungu, hali yangu kama mnavyoniona, naendelea vizuri sana. Nilivyo sasa si sawa na nilivyokuwa awali kabla ya kwenda India kupatiwa matibabu.
AWAKUMBUKA WATANZANIA
Sajuki aliwashukuru Watanzania waliomchangia fedha, maombi na dua akisema mambo hayo ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya afya yake ifikie ilipo sasa.
AWASHUKURU WALIOMZUSHIA KIFO
Aidha, Sajuki hakusita kuwashukuru wale wote waliotumia muda wao mwingi kutangaza kwamba yeye amefariki dunia kutokana na maradhi yake.
“Hata wale waliotumia muda wao mwingi kutangaza kwamba mimi nimefariki dunia, pia nawashukuru na Mungu awazidishie. Huenda walifanya vile kwa kuamini walichokuwa wanakifanya ni sahihi.”
WALIODAI UGONJWA WAKE NI ADHABU YA UTAPELI JE?
Sajuki alikwenda mbele zaidi kwa kusema katika maisha yake hajawahi kumtapeli mtu, lakini aliposikia kuna watu wanazusha ugonjwa wake ni adhabu kutoka kwa watu aliowatapeli alishangaa sana.
“Mimi sijawahi kumtapeli mtu, siku zote nakula kwa jasho langu. Lakini nikiwa India nilisikia eti naumwa kwa sababu niliwatapeli watu kwa hiyo waliniadhibu, nilishangaa sana! Lakini nasema hivi, hata wao nawashukuru kwa yote, Mungu awazidishie.”
WASTARA NAYE BWANA, AANGUSHA NENO ZITO
Asema: “Kuna watu wananikataza nisiseme ukweli kuhusu afya ya mume wangu eti atazidiwa zaidi, mimi nasema simuogopi mtu yeyote kwani kama ni uchawi mimi ni mchawi zaidi yao.
“Mimi naroga kutwa nzima kwa mtu mmoja tu ambaye ni Mwenyezi Mungu, lakini wao wanaroga usiku tena wakiwa na shaka hivyo sitaacha kusema mume wangu anaendelea vizuri kama hivi alivyo sasa.”
KISA CHA KUFIKA HAPA
Sajuki alianza kuugua mwaka jana ambapo alipata matibabu kwenye Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam na kubainika ana uvimbe tumboni. Hata hivyo, afya yake ilizidi kwenda mrama na kusababisha kushindwa kutembea.
Wadau, mashabiki wake, ndugu jamaa na marafiki walianza ‘kampeni’ ya kumchangia fedha ili apelekwe kutibiwa nchini India ambapo Mei, 2012 alisafirishwa kwenda nchini humo na kufanyiwa upasuaji.
Sajuki alirejea nchini baada ya wiki mbili lakini hali yake ilikuwa si ya kuridhisha huku akiendelea kutumia dawa

12:08 AM | Posted in | Read More »

TANZANIA YAPANDA NAFASI 12 ZAID JUU.

Tanzania (Taifa stars) imepanda hadi kufikia nafasi ya 127 kutoka nafasi ya 139, huku ivory coast ikishika nafasi ya 16 Dunian. Mabigwa wa kutandaza kabumbu Spain ikishika nafasi ya 1, waandaaji wa kombe la dunia Brazil wa kishuka hadi nafasi ya 11 kulingana na viwango vya FIFA.

12:05 AM | Posted in , , | Read More »

CHUZ,ROSE WA CHUZ WAMWAGANAHATIMAYE ule uchumba wenye makeke wa Mkurugenzi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ na msanii wa kundi hilo, Rose Michael ‘Rose wa Chuz’ umekatika na wawili hao wamemwagana, Risasi Mchanganyiko lina ushahidi mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wamemwagana kufuatia timbwili zito aliloliangusha Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ nyumbani kwa Chuz hivi karibuni akimtuhumu demu huyo kumtesa mwanaye wakati baba mtu alipokuwa Zanzibar ‘Zenji’ akirekodi filamu ya Dirty Game.
Habari zinasema baada ya Chuz kurejea kutoka Zenji, Rose alitoa dukuduku lake kwamba, hawezi kuendelea kulea ‘toto ambalo’ mama yake hana shukurani.
“Kisa cha hawa watu kumwangana ni Jini Kabula, Chuz alikwenda Zenji kushuti filamu, aliporudi akakuta Rose amevimba macho kwa kulia, alipoulizwa kasema Jini Kabula alimfanyai fujo akimtuhumu kumtessa mwanaye.
“Chuz alijaribu kumlainisha Rose kwa maneno ‘matamtam’ lakini hakukubali, akaondoka kurudi kwao Arusha, hivi leo (juzi, Jumatatu) ninavyoongea na wewe, Rose yupo Arusha kwa wazazi wake,” kilisema chanzo hicho.
Paparazi wetu alimsaka Chuz kwa simu ya kiganjani na alipopatikana na kusomewa mashitaka yake, alikuwa na haya ya kusema:
Chuz: Aaah! Kifupi ni kwamba, ‘asa hivi mi naangalia kazi bwana. Unajua filamu za Bongo zinauza sana, lakini hata hivyo, tumejitahidi kuwa kama Wanaijeria, si eti?”
Risasi Mchanganyiko: Jibu swali langu, ni kweli umemwagana na Rose?
Chuz: Rose yupo, unajua yule demu (Rose) atakuja kuwa staa mkubwa sana haba Bongo, mi nakwambia. Anajua kuuvaa uhusika katika filamu. Ha! Ha! Ha! Ha!
Rose alipopigiwa simu siku ya Jumatatu iliyopita hakuweza kupatikana mara moja hewani.
Mapema mwaka huu, moja ya magazeti ya Global Publishers liliripoti Chuz kutangaza hadharani kwamba Rose ni mchumba wake na wangefunga ndoa katikati ya mwaka huu. Aliongeza kuwa msichana huyo ndiye mwanamke wa maisha yake baada ya wote waliopita.
Hata hivyo, Gazeti la Amani likaja andika habari zilizotoka kinywani mwa Jina Kabula akimuasa Rose kuwa makini na Chuz kwamba katika wanaume waongo ulimwenguni, jamaa huyo anashika nafasi ya pili.
Mbali na Rose, Chuz ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Joan Mutovolwa, Leila Ismail ‘Lilly’ (amezaa naye) Miriam Jolwa Jini Kabula (amezaa naye).

11:01 AM | Posted in , | Read More »

Timu ya Gyan Asamoah yamwaga Sh 160mKiungo mpya wa Yanga, Nizar Khalfan.
Na Saleh Ally
Klabu ya Al Ain ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), imesema ipo tayari kumsajili kiungo mpya wa Yanga, Nizar Khalfan, kwa kutoa dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 160), bila kuchelewa.
Al Ain ndiyo timu ya Uarabuni anayoichezea mshambuliaji nyota raia wa Ghana, Asamoah Gyan ambayo ilimchukua kwa mkopo kutoka Sunderland ya England na kulipa ada ya pauni milioni 6 (zaidi ya Sh bilioni 15).
Mmoja wa maofisa wa Al Ain, Mohammed Ismail, ameliambia Championi Jumatano kuwa wamefanya mawasiliano na Yanga kuhusiana na kumtaka Nizar.
“Tumewaambia kuwa tunamhitaji na tupo tayari kulipa kiasi hicho, wakiwa tayari basi tutampokea. Tunahitaji viungo ili wasaidie mashambulizi, pale mbele tunaye Gyan Asamoah, nafikiri unajua hilo,” alisema Ismail.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa tayari suala hilo limewasili ndani ya Yanga na Nizar amekwishapewa taarifa lakini inaonekana hana mpango wa kuiacha Yanga ambayo amejiunga nayo hivi karibuni baada ya kuachwa na Klabu ya Philadelphia Union ya Marekani.
“Kweli tumepata hayo maombi, lakini ni suala ambalo lipo chinichini. Zaidi tunaangalia kwanza, maana Nizar tunamhitaji na hatujui yeye anahitaji nini, lakini jamaa wameahidi kutoa mshahara mnono,” kilieleza chanzo.
Al Ain ni miongoni mwa timu tajiri na hivi karibuni ilitangaza nia ya kumbakiza Asamoah kwa kutoa ofa ya euro milioni 60 (Sh bilioni 120) na mshahara wa euro 250,000 (Sh milioni 500) kwa wiki.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Nizar alisema alipata taarifa kuhusiana na dili hilo lakini hajakaa chini na viongozi wake.
“Kweli nilisikia taarifa kuhusiana na hilo, nimeambiwa na mmoja wa viongozi lakini haikuwa rasmi sana,” alisema Nizar ambaye alisisitiza asingeweza kulizungumzia zaidi hadi atakapopata taarifa za uhakika.
Iwapo Nizar atakubali kuondoka na Yanga ikaona hakuna ‘gogoro’, mchezaji huyo atapata nafasi ya kucheza kikosi kimoja na Asamoah.
Al Ain inaona sahihi kumbakiza Asamoah baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa wa 10 wa ligi ya UAE huku akiwa amefunga mabao 22 katika mechi 18 alizocheza katika mashindano yote.
Klabu hiyo imekuwa ikitaka kujiimarisha zaidi na wachezaji kadhaa nyota kama Abedi Pele (Ghana), Hossam Hassan (Misri), Mustapha Hadji (Morocco),

10:58 AM | Posted in , , | Read More »

Lulu Achimba Mkwara Mzito Mahakamani


MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amechimba mkwara mzito katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, Risasi Mchanganyiko linatiririka.
Lulu ambaye ni mshukiwa namba moja wa kifo cha msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, alichimba mkwara huo, juzi Julai 02, mwaka huu wakati akifikishwa mahakamani hapo, kesi yake inapoendeshwa.
ATEMA CHECHE
Baada ya Lulu kushuka katika gari la Magereza na kusindikizwa kwenda kizimbani na askari Magereza, alianza kumshambulia mwandishi wetu kwa maneno alipomuona amekazana kupata picha zake.
“Hivi hamchoki kunifuatafuata? Kila siku Lulu, Lulu niacheni na maisha yangu! Kwani kuna kitu gani kipya tena?
“Hivi nyie hamna kazi nyingine ya kufanya...baba mzima unahangaika kunifuatilia? Nimechoshwa na tabia yenu bwana,” alibwatuka Lulu bila woga.
ASKARI WAPIGWA NA BUTWAA
Wakati Lulu akitema cheche, askari waliokuwa ‘wakimueskoti’ walibaki wamepigwa na butwaa bila kuamini kama ni kweli Lulu ndiye aliyekuwa akizungumza kwa ujasiri mkubwa kiasi kile.
Mdau mmoja aliyekuwepo mahakamani hapo, alisikika akisema: “Mh! Mwanzoni Lulu alikuwa analia kila siku, lakini sasa naona ameanza kuzoea...amekuwa mbogo huyo!”
KESI YAKE NENDA RUDI
Kesi ya Lulu imeonekana kuwa na mvutano mkubwa huku matumaini ya kuanza kusikilizwa yakionekana kuwa hafifu kutoka na shauri hilo kuendeshwa katika mahakama mbili tofauti.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo, Elizabeth Kaganda, mbele ya Hakimu Agustina Mbando alisoma kesi hiyo lakini kabla ya mtuhumiwa hajajibu chochote, hakimu aliihairisha kesi hiyo.
Hakimu Mbando alisema, analazimika kuhairisha kesi hiyo hadi Julai 16, mwaka huu kwa vile shauri hilo halijakamilika kwa sababu lipo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ikijadiliwa suala la umri.
Hata hivyo, mahakama kuu ilipeleka shauri hilo katika mahakama ya rufaa baada ya mawakili upande wa serikali, kupinga suala la umri wa Lulu kujadiliwa mahakamani hapo, badala yake lipelekwe katika mahakama ya rufaa.
Mawakili hao walisema, kwa sasa Lulu atabaki kujulikana kuwa ana umri wa miaka 18, ambao aliandikisha yeye mwenyewe katika Kituo cha Polisi Oysterbay alipokuwa akihojiwa kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa.
NDUGU, WASANII WAMTOSA
Aidha, siku hiyo hakukuwa na ndugu yeyote wa Lulu wakiwemo wazazi wake aliyefika mahakamani hapo kufuatilia shauri hilo.
Ukiachilia mbali hao, hata wasanii wenzake ambao wana jumuiya mbalimbali kama Bongo Movie na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) pia hawakufika kumuona mwenzao.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Lulu alikamatwa Aprili 07, mwaka huu kwa madai ya kuhusika na kifo cha marehemu Kanumba, kilichotokea nyumbani kwake, Sinza - Vatican, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia siku hiyo.
Kwa sasa yupo katika Gereza la Segerea huku kesi yake ikiendelea kuunguruma katika mahakama mbili tofauti; Hakimu Mkazi, Kisutu na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

10:51 AM | Posted in , | Read More »

Diamond Apagawisha Songea-Show Yavunja Record


SHOO ya  nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo Naseeb Abdul 'Diamond' imeingia katka kitabu cha matukio yaliyokusanya watu wengi zaidi katika historia ya mji wa songea  na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Akizungumza na Teentz.com mapema leo Mkurugenzi wa Jambo Lee Club  ambayo iliratibu ziara nzima ya mwanamuziki huyo amesema kuwa shoo ya Diamond imevunja rekodi na kuingia kwenye kumbukumbu za watu  kwa kujaza watu wengi na pia  ikiwa ni shoo pekee iliyokuwa na msismko mkubwa  kuliko hata inavyokuwa  wakati wa michezo ya soka inayozihusisha timu kubwa na Simba na Yanga zinapokuja kucheza Songea.
"Shoo imefunika hakika haijawahi kutokea, watu kujaa kwa wingi kiasi kile katika  shoo za muziki hii imevunja rekodi, kwa kweli kama waratibu tumefarijika sana kuona  watu wamejitokeza kwa wingi, kwani hatukutegemea ingawa msisimko uliokuwepo kabla ulikuwa mkubwa kuliko hata ule unaokuwepo wakati Simba na Yanga zikija kucheza hapa Songea" alisema Mukugenzi huyo.

10:43 AM | Posted in , | Read More »

KANYE WEST, JAY – Z, BIG SEAN CHRISS BRIZZ WATISHA B.E.T 2012.

.
Usiku wa Jumapili iliyopita Big Sean aliperform kwenye tuzo za B.E.T na Kanye west 2 Chainz na Pusha T. Alipata tunzo ya Best New Artist, Jay – z na Kanye West wakachukua tunzo ya Video of the year “Ortis” Diggy Simmons alichukua tunzo ya Younstar Award, Chriss Brown alichukua tunzo ya “Best Male R&B Artist Msanii mburudishaji wa mwaka. Beyonce alishinda tuzo ya Video Director wa mwaka akiwa na Alan Ferguson na ngoma ya “Party” na Best Female R&B Artist wakati Wale na Miguel wakashinda tuzo ya “Lotus Flower Bomb”  na Nick Minaj alishinda kama Best Female Hip-Hop Artist.
Kama vipi check list nzima chini :-

Centric Award
Common
Younstars Award
Diggy
Best Group
The Throne (Jay-Z and Kanye West)
Best Actor
Kevin Hart, "Think Like a Man"
Best New Artist
Big Sean
Best Male R&B Artist
Chris Brown
Best Collaboration
Wale (featuring Miguel), "Lotus Flower Bomb"
Best Gospel
Yolanda Adams
Best Female R&B Artist
Beyoncé
Best Female Hip-Hop Artist
Nicki Minaj
Lifetime Achievement Award
Maze, featuring Frankie Beverly
Video of the Year
The Throne (Jay-Z and Kanye West), featuring Otis Redding, "Otis"
Humanitarian Award
The Reverend Al Sharpton
Viewers' Choice Award
Mindless Behavior
Video Director of the Year
Beyoncé and Alan Ferguson
Entertainer of the Year
Chris Brown

10:40 AM | Posted in , | Read More »

Facebook boss Got Married ( Boss wa Facebook aoa mwanaume mwenzake)

.
Baada ya mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa facebook Chris Hughes kufunga ndoa ya jinsia moja na mpenzi wake wa muda mrefu bwana Sean Eldridge jumamosi iliyopita huko New York City, USA last Saturday, the social networking website chose to symbolically introdMtandso huo umeamua kuongeza kitufe kitakacho ashiria ndoa za jinsia moja kwenye relationship status za mtandao huo.
Kwa kawaida ilikua mtu akioa kwenye page yake ya facebook anaruhusiwa kubadilisha status ambapo kitufe cha facebook huwa kinaonyesha mwanaume na mwanamke lakini kwa sasa inaweza kuwa mwanaume kwa mwanaume au mwanaume kwa mwanamke.
Hiki ndio kitufe walichokiongeza kwenye facebook cha ndoa ya wanaume waliooana.
Mabadiliko haya sio mapya kwenye mtandao wa facebook katika harakati za kwenda na wakati kwani 2011 facebook iliongeza kitufe cha kuonyesha kwamba ndoa imefungwa mahakamani hatua ambayo ilionekana kuunga mkono ndoa za kimahakama za watu wa jinsia moja.
Pamoja na hilo facebook imekua inatoa support kwa asasi zisizo za kiserekali ambazo zimekua zikiweka kipaumbele kwenye kutetea haki za mashoga na wasagaji.

10:38 AM | Posted in , | Read More »

Kocha Mpya wa Yangu Huya hapa


10:34 AM | Posted in , , | Read More »

Uwoya na Flora Mvungi Wapakana Kisa H-Baba
MASTAA wawili wanaokimbiza kwenye sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Flora Mvungi hivi karibuni wamevunjiana heshima kisa kikiwa ni msanii wa Bongo fleva, Hamis Ramadhani Baba ‘H. Baba’ Risasi Jumamosi linakujuza.
Akizungumza na gazeti hili, Flora ambaye anatoka na H. Baba hivi sasa, alionesha kukasirishwa na kitendo cha Uwoya kumtolea kashfa mwanaume wake huyo mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kwa kusema kuwa hayajui mapenzi.
HUYU HAPA UWOYA 
Katika mahojiano aliyofanya na jarida moja la burudani hivi karibu, Uwoya bila ya kuumauma maneno, alishusha tuhuma nzito kwa H. Baba ambaye alikuwa mwandani wake wa zamani na kumchana kwamba ni ‘mbumbumbu’ anapofika kwenye kiwanja cha sita kwa sita ndiyo sababu penzi lao likavunjika.
FLORA ANATIRIRIKA
“Anadai H. Baba hajui mapenzi wakati miye ndiyo nimefika, ananiridhisha vya kutosha! Yeye ndiyo hajui mapenzi ndiyo maana hakai na wanaume kila siku anamzungumzia H. Baba. Atakuwa bado anamtaka angekuwa muwazi, asingekuwa anamzungumzia kila siku.
“Kuna raha anazozikumbuka ndiyo maana anaongea sana. Wanaume wote aliotoka nao mbona hawazungumzii? Aseme anachotaka asizunguke,” alisema kwa hasira.
Frola anadai kuwa Uwoya roho inamuuma kwa kuwaona wawili hao wanavyopendana, kama vile haitoshi Frola alisema kuwa Uwoya hawezi kuishi na mwanaume ndiyo maana hata ndoa yake imemshinda.
“Si aliolewa na anayedhani anajua mapenzi, mbona kashindwa kudumu naye?” alihoji Frola.
NI KWA NINI H. BABA?
Kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita inaonesha, Uwoya aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na H. Baba wakamwagana, hivyo imedaiwa kuwa hafurahi kumuona Flora akifaidi mapenzi motomoto ya H. Baba.
KUMBE NI VITA YA MUDA MREFU
Mbali na Uwoya ‘kumvua’ vibaya H. Baba kwenye jarida hilo kwamba hajui mapenzi, chanzo makini kimeeleza kuwa mara kwa mara Uwoya amekuwa akimtupia vijembe vya dharau Flora kwamba amejiweka kwa mtu ambaye hajui mapenzi.
“Siyo mara moja wala mara mbili, Uwoya anawadharau sana H. Baba na Flora hata hivi majuzi amewachana redioni,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini.

8:54 AM | Posted in , | Read More »

Mwanamuziki Pipi Aonyesha Picha za Ujauzito Wake


Mwanamuziki wa kike nchini Tanzania aliyewahi kutamba na wimbo ‘Njia Panda’, Doreen Aurelian Cassian Ponera aka Pipi, ameamua kuweka wazi furaha aliyonayo kwa kuwa mama mtarajiwa.
Pipi ambaye kwa sasa ana wimbo mpya uitwao ‘Unapokuwa mbali’ ameyaondoa mashaka waliyokuwa nayo baadhi ya watu walioiona video hiyo na kugundua kuwa kuna mabadiliko kwenye saizi ya tumbo lake na hivyo kuhisi kuwa tayari ni mjamzito.
Jana kupitia Facebook ameamua kuonesha live tumbo lake na kuwapa jibu wale walioukuwa na mashaka na hali yake ya sasa.
Kitendo chake cha kuwa wazi kiasi hicho na kujivunia kuwa mama mtarajiwa, kimesifiwa na watu wengi.
“It’s hard kwa wanawake wengi kudisclose their affairs especially pregnancy but umeweza, unastahili pongezi kwa kweli, kwanza kwa kukubali kuitunza mpaka hapo maana wengi hupendelea abortion,” aliandika mmoja wa rafiki zake.
Nasi pia baada ya kuona picha hizo tulimtupa pongezi kwa ujasiri huo kwa kumwambia, “Naona you are a proud mama to be! Hongera sana,” na yeye akajibu, “Hahaha, yes am very proud, thanks a lot!

8:46 AM | Posted in , | Read More »

Alpha: Milioni tisini za TPF3 bado unataka uendelee kushikwa mkono?


Wiki hii mshindi wa Tusker Project Fame msimu wa tatu Alpha Rwirangira wa nchini Rwanda ameandika barua ndefu kuishutumu kampuni ya East Africa Breweries Limited, EABL, kuwa imeshindwa kuwaunga mkono washindi waliopita baada ya show.
Barua yenyewe iliandikwa hivi:
“Naandika barua hii nikiwa na uchungu mkubwa moyoni. Mashabiki wangu wapendwa, inauma sana. Kwanza naishukuru EABL kwa kunitambulisha kwenye midani ya muziki. Lakini niruhusuni tena niseme kukatishwa kwangu tamaa.
EABL inaingiza hela nyingi sana kutokana na washiriki hawa lakini bado haitaki kuwaunga mkono na kuwajali baada ya show. Ningependa kuwapa mfano wa Victoria Kimani, kama angekuwa mkweli na kuwaambia yote aliyoyapitia baada ya kushinda TPF1, ni aibu sana, kama EABL ingekuwepo kwaajili yake ninaamini Kimani angekuwa mbali sana na kipaji chake.


Mwangalie Ester, ni aibu jinsi watu wengi wasivyojua kuhusu yeye na bado hawamjui mwimbaji huyu mwenye kipaji, natamani angesimulia story yake kutokana na njia aliyoipitia baada ya TPF2, ni aibu kubwa.
Sasa kuhusu mimi, ni story ile ile naomba radhi kwa kusema hilo, hata hivyo sina cha kupoteza lakini EABL hili ni kubwa mnahitaji kuwasaidia wasanii wenu, msiwaache wakirandaranda kama kondoo waliopotea.
Mnachofikiria ni kuhusu ninyi wenyewe, inauma sana. Nakumbuka niliandaa show nyumbani Rwanda ambako nilileta baadhi ya wahusika wa TPF akiwemo jaji Ian, na niliwaomba EABL wadhamini show yangu wakapuuzia baada ya kuwaonesha ni kiasi gani ninajituma angalau kuwa mbunifu na kufanya nao kazi.
Ni aibu kwamba nilidhaminiwa na makampuni mengine na EABL haikuwepo licha ya kuwa niliwafuata kuwaomba udhamini kama makampuni yote haya mengine. Waliendelea kunipa ahadi mpaka dakika ya mwisho, ni aibu na inauma.
Na sasa mwangalie kaka yangu Davis, mpaka sasa hivi anahangaika na record deal, EABL sijui kinachoendelea kwenye mkataba wake kwakuwa hakuna kilichofanyika hadi sasa na TPF 5 inaendelea, unadhani watu hawa wanawatendea haki wasanii? Ninashangaa kwanini wanaendelea na TPF5 kama watakuja kufanya sawa na walivyotufanyia sisi sote? Sio haki.
Tafadhali watu msinielewe vibaya lakini watu huwapigia kura wasanii wawapendao na wanapenda kuwaona wakikua na wasipoona kile walichotarajia huwalaumu wasanii, tafadhali naomba mniruhusu kuwaonesha akina nani wanaopaswa kulaumiwa.
Inauma sana. Nimeviweka vitu moyoni mwangu lakini umefika muda niviseme, kwakuwa sina cha kupoteza lakini walau wacha niongee na wadogo zangu ili wasije kukutana na tatizo lile lile. Tafadhali mashabiki wetu tunaomba maoni yenu kuhusu suala hili.”
Maoni yetu
Kwanza kabisa tungependa kukubaliana na madai yake hayo dhidi ya waandaji wa Tusker Project Fame kwakuwa wanawajibika kuhakikisha kuwa washindi waliopatikana wanapewa uwezo wa kuja kupambana na wasanii wengine waliotoka kwa njia ya kawaida.
Barua ya Alpha imetukumbusha makala tuliyowahi kuiandika hapa Bongo5 kuhusiana na jinsi mashindano mengine kama hayo ya hapa Tanzania, Bongo Star Search yanavyotoa washindi wasioweza kumudu ushindani wa muziki. Barua hiyo ikatuamsha kuwa kumbe pamoja na mbwembwe zote hizo za TPF, hawachekani na BSS. Wote wale wale. Hutoa washindi ‘vibogoyo’ wasioweza kumudu soko la muziki baada ya kutoka huko.
Aliyoyasema Alpha kuhusiana na ukimya wa washindi wote wa awali wa mashindano hayo ni kweli. Ukianza na Victoria Kamani, leo hii ukiwauliza watanzania mia moja tena wale wapenzi wa muziki, huenda mmoja tu ndo anaweza kuwa anamfahamu.
Kwanini hafahamiki? Well, sababu ya Alpha ni kuwa EABL imeshindwa kumsupport! Swali kwa Alpha ni kuwa, mbona kuna vijana wanafanya muziki katika mazingira magumu kabisa lakini wanafanikiwa. Wapo waliotoka bila msaada wa maana kutoka kwa mtu ama kampuni. Wapo waliotoka mikoani na shilingi laki mbili tu za kurekodia wimbo na kulala kwa washkaji zao Dar es Salaam, lakini leo ni masupasta hata kama hawana kipato kikubwa kivile, kama mtu huyu anavyosema kumjibu Alpha, “Kaka well use the example of your cousin AY. He hustled his way out through the industry and got to make it big. EABL gave you a shortcut to being there in two months and gave you a big fund that most East African artists could hardly make in their early stages of music career! ‘
They prepare you enough for the competition out here I believe. What you got to do now is simply focus ahead and not drain your energy blaming boss wa jana! Instead muonyeshe uwezo wako by opening kampuni yako leo! So wewe kamua huko CA upae zaidi!”
Kwanini hawa akina Alpha ambao kwanza hupewa airtime kila weekend wakati wa mashindano hayo kwa kuonekana live wakiimba kwenye TV, lakini wakipata ushindi na kupewa kitita cha mamilioni ya shilingi hushindwa kufanya lolote.
Alpha alipewa zawadi pamoja na mambo mengine, shilingi milioni tano za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni tisini za Tanzania. Hela zote hizo na bado anataka EABL waendelea kumshika mkono?
“Please Alpha, don’t mislead the people.. They did what they were supposed to do and it is puting you and your colleagues in the limelight, now it’s up to you and no one else.. And for the sponsoring a show part, that’s very different and the have all the rights to accept or decline. Dont mislead us please,”aliandika mtu mmoja chini ya barua hiyo ya Alpha aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Mwingine aliongeza, “Tusker project fame is a Launchpad, they promise the winner %5million which they give, they don’t promise to offer any other support like sponsoring events. There are so many people who need that exposure they gave you…. It’s the artist duty to work hard after TPF…. EABL is not a Musician nurturing company…If an artist doesn’t work hard after tpf, they can’t breast feed them.”
Akiwa na milioni tisini alikuwa na uwezo wa kurekodi wimbo sehemu yoyote anayotaka na kufanya video nzuri. Ama hela zimeshaisha na sasa anataka EABL wamwongezee zingine? Huo utakuwa ni mchezo wa pwagu na pwaguzi wa kusindikizana siku nzima.
Labda cha maana sana ambacho EABL na TPF wanapaswa kufanya sasa hivi ni kuwajengea washiriki uwezo wa kujitegemea na kusimama wenyewe watokapo kwenye mashindano hayo. Kamwe hawawezi kufanikiwa kama wasanii wenyewe watakuwa wakitegemea walishwe kila kitu.
Leo hii washindi waliopita wakiwemo Esther na Davis wa Uganda ni kama wanatakiwa waanze tena upya kama underground! Watu wamewasahau. Jambo linalotushangaza ni kuwa mbona wakati wakiimba kwenye mashindano hayo walionesha vipaji vya hali ya juu kuzidi hata wasanii wengi wakubwa waliofanikiwa?
Wanapokuja huku nje, nini hutokea? Ama ni ngumu sana kwa msanii aliyeshiriki mashindano ya vipaji kukubalika kwenye mainstream music? Majibu ya maswali haya ni magumu mno kuyapata.
Ushauri kwa Alpha na washindi wengine wa TPF ni kuwa wakubali sasa hivi wapo wenyewe na wanatakiwa kuhangaika kivyao.Muda wa kulishwa na wao kumeza tu ulishaisha tangu washinde. Wajifunge kibwebwe hasa kupambana na wasanii wengine waliotoka kawaida.
Bila hivyo wataendelea kulalamika maisha yao yote. Endelea kusonga mbele kama ulivyowahi kuimba and be man! The strongest man in the world is the man who stands alone.

8:45 AM | Posted in , | Read More »

Bob Junior kufunga ndoa Billicanas July Mosi


Mwanamuziki na producer anayemiliki studio ya Sharobaro Records, Bob Junior aka Mr. Chocolate Flava, ameamua kufungua ndoa kwa style ya aina yake.
Amesema harusi yake itakayofanyika jumapili ya tarehe moja mwezi July mwaka huu, pamoja na kufanyika nyumbani itatinga ndani ya club ya Billicanas ambapo kila mtu anaruhusiwa kuhudhuria.
Rais huyo wa masharobaro amesema wiki hii atapanda boti hadi Zanzibar kwenda kumfuata ‘mwali’ ili aisaliti rasmi kambi maarufu ya makapela.
Bob Junior anayesifika kwa kukata ‘mauno’ kwenye video zake, amesema amechoka kuishi maisha ya ujana na sasa anahitaji kuwa na familia.
“Tunapiga show kila siku na kupata hela nyingi kwanini nisioe,” aliiambia 255 ya Clouds Fm jana.
Aliongeza kuwa dhumuni la kuamua kuoa ni kuepukana na vishawishi na maradhi kwakuwa watu maarufu kama yeye hujikuta wakitafutwa sana na wasichana.
Kila lakheri Bob Junior.

8:42 AM | Posted in , | Read More »

Drogba sasa huenda akatua BarcaDIDIER Drogba anaweza kufanya uhamisho wa kushangaza kuhamia Barcelona ya Hispania ikiwa ni muda mfupi tangu kusaini mkataba wa kuichezea timu ya  Shangha Shenhua ya China.
Nyota huyo wa Ivory Coast, aliachana na klabu yake ya Chelsea aliyoiwezesha kutwaa taji la Klabu Bingwa Ulaya na kuamua kwenda China.
Alitarajia kwenda mjini Barcelona kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Wakurugenzi wa klabu hiyo. Mazungumzo hayo yalipangwa kufanyika Jumanne wiki hii.
Drogba (34) alitarajia kulipwa mshahara wa pauni 200,000 (Sh483 Milioni) kwa wiki na klabu hiyo ya China.
Aliposaini alisema: "Nathibitisha nimesaini kucheza klabu ya Shanghai Shenhua ya China kwa miaka miwili na nusu. Nitarejea kujiunga na klabu Julai.
"Nimetafakari ofa zote nilizopewa wiki kadhaa zilizopita, lakini nadhani Shanghai Shenhua ni sehemu sahihi kwangu kwenda kwa muda huu.
"Najiandaa kukutana na changamoto mpya na kujifunza utamaduni mpya pia. Lakini pia nafurahia kusikia maendeleo ya Ligi Kuu China.
"Chelsea ilipokwenda China mwaka jana, tulikuwa na fursa nzuri na mashabiki walitufurahia. Natarajia kuitangaza ligi ya China duniani kote," alisema Drogba.

11:16 PM | Posted in | Read More »

Kocha mpya Yanga mambo safi


Clara Alphonce na Jessca Nangawe
MABINGWA  wa Kombe la Kagame, Yanga ya jijini Dar es Salaam, watamtangaza kocha wao mpya Ijumaa wiki hii, ambapo ataanza kazi rasmi mara baada ya michuano ya Kombe la Kagame baadaye mwezi ujao.
Kwa maana hiyo, Kocha Msaidizi, Fred Minziro ndiye atakayeketi kwenye benchi na kuiongoza timu hiyo inayovaa jezi za rangi ya njano na kijani kutetea taji hilo.
Awali, Yanga ilibainisha kuwa inasaka kocha mwenye uzoefu na soka la Afrika pamoja na mazingira yake kama ilivyokuwa kwa kocha aliyeondoka, Kostadin Papic raia wa Serbia.
Kiongozi wa usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.
Na kwa upande wa Katibu wa Yanga, Selestine Mwesigwa ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kwa sasa, alisema kuwa majina ya makocha watatu yameshapitishwa.
"Kulikuwa na maombi ya makocha 25, baada ya mchujo tumechagua makocha watatu ambao tunawachuja na kumtangaza mmoja wiki hii," alisema.
Alisema timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kaunda tayari kwa maandalizi ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza Julai 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo, Kelvin Yondani aliyejiunga Yanga toka Simba, amesema katika kipindi kifupi alichofanya mazoezi klabu yake hiyo mpya, amebaini kuwa hakufanya makosa kutua Jangwani.
Yondani alisema kuwa, maisha ya Jangwani ni mazuri hasa ukizingatia kuwa amepata mapokezi na ushirikiano mzuri na wachezaji na viongozi.
Pia ametumia fursa hiyo kuitaka Simba kumsahau kwani yeye tayari ni mali ya Yanga na hakuna jitihada zozote za kujaribu kumrudhisha Simba zitakazofanikiwa.
Uhamisho wa Yondani ulizua utata mkubwa baada ya klabu yake ya zamani kudai ni mchezaji wao halali, huku Yanga na mchezaji wenyewe wakisema tofauti.
"Sifahamu kwanini Simba bado wanazungumza mambo haya. Mimi nimeshamaliza kila kitu na Yanga, ni vizuri wakaniacha nifanye kazi Yanga," alisema Yondani.

11:13 PM | Posted in | Read More »

Bilioni 300 za vigogo Uswisi zatikisa nchi


Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Zitto Kabwe
ZITTO AMTAKA PINDA ATAJE WAHUSIKA, WANANCHI WATAKA FEDHA ZIREJESHWE, MABILIONI ZAIDI YAIBWA MTANDAONI
KUBAINIKA kwa Sh303.7 bilioni zilizofichwa katika akaunti za vigogo wa Serikali na wanasiasa nchini Uswisi, kumetikisa nchi huku shinikizo likitolewa kwa vyombo vya dola kuchunguza haraka na kuchukua hatua za kisheria, ikiwamo kurejesha fedha hizo.

Jana kutwa nzima, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa wasomaji wake wakiwamo wabunge na mawaziri, huku baadhi wakichangia maoni kwenye tovuti na mtandao mbalimbali ya kijamii, wakitaka kujua majina ya wamiliki wa akaunti hizo.

Bungeni mjini Dodoma, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuchunguza tuhuma hizo kisha kuwachukulia hatua watu sita wanaotajwa kwamba wanamiliki akaunti zenye mabilioni hayo ya shilingi chini Uswisi.

Fedha hizo zimebainishwa na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB), iliyotolewa hivi karibuni, ikitaja nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, na kiwango cha fedha zilizohifadhiwa huko.
 
Tayari Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kimeeleza kuwapo kwa fedha hizo katika benki mbalimbali nchini Uswisi, zilizoingizwa na kampuni za uchimbaji mafuta na madini.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nayo imeweka bayana kuwa inafuatilia suala hilo kwa mamlaka za Uswisi, ili kujua fedha hizo ziliko na nani anazimiliki. 

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zina fedha nyingi katika benki za Uswisi ni Kenya (dola 857 milioni), Uganda (dola 159 milioni), Rwanda (dola 29.7 milioni) na Burundi dola 16.7 milioni.

Chanzo cha habari hizo, kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi moja.

Kauli ya Zitto

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, aliliambia Bunge jana kuwa haiwezekani nchi ikaendelea ilhali watu wanakusanya fedha kutokana na utafiti wa gesi na mafuta, ambao bado haujaanza kulinufaisha Taifa.
 
Akichangia Bajeti ya Waziri Mkuu, Zitto alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) ielekezwe ili ifanye uchunguzi utakaowezesha wamiliki wa akaunti hizo kufahamika, ili wachukuliwe hatua mara moja bila kujali nafasi wanazozishikilia ndani ya Serikali.
 
“Viongozi wanaohamisha na kupeleka fedha za Watanzania nje ya nchi wanatakiwa wachukuliwe hatua mara moja. Hili litatusadia katika siku zijazo, kwani kama wapo wengine wanaodhani wanaweza kuficha fedha zao nje basi wajue kwamba popote watakapozipeleka tutazifuata na kuzirejesha,” alisema Zitto na kuongeza;

“Namuomba Waziri Mkuu aagize uchunguzi ufanyike, fedha hizi zirejeshwe na wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Zitto.
Zitto alitoa kauli hiyo akiyanukuu magazeti ya Mwananchi, The Citizen na The East African ambayo kwa nyakati tofauti yameandika kuhusu kuwapo kwa kiasi kikubwa cha fedha zinazotokana na rushwa, ambazo zimehifadhiwa kwenye akaunti kadhaa nchini Uswisi.
 
Alisema kuachia suala hilo kuendelea ni hatari, kwani uchumi wa nchi utahujumiwa hata kabla ya miradi husika haijaanza kutekelezwa.
 
“Haiwezekani sisi tupo tunahangaika kutafuta gesi na mafuta huko baharini Lindi na Mtwara, halafu watu wengine tayari wameishawekewa hela kwenye akaunti, kwa hakika lazima uchunguzi ufanyike na watu hawa wajue kwamba Serikali ina uwezo wa kuwafahamu na kurejesha hizo fedha hizo nchini,” alisema Zitto.
 
Alitoa mfano wa Serikali ya India ambayo iliwahi kupata taarifa za baadhi ya watumishi wake kuficha fedha nchini Uswisi na kuchukua hatua za kiuchunguzi zilizowezesha wahusika kutajwa hadharani, kisha fedha zilizoibwa serikalini kurejeshwa.
 
Katika hatua nyingine, Zitto alitaka mvutano baina ya Tanzania Bara na Visiwani kuhusu masuala ya gesi umalizwe ili kuwezesha utafiti kuendelea kufanywa katika maeneo ya bahari ya Hindi.
 
Alisema utafiti katika baadhi ya maeneo hasa eneo la Bahari karibu na kisiwa cha Pemba umesimama kutokana na mvutano wa iwapo suala la mafuta ni la Muungano au la.

“Kama visiwani watavumbua gesi ni sawa, wavumbue kivyao, na sisi Tanzania bara tumeshavumbua matrilioni ya gesi, basi tuendelee kivyetu lakini tusisimamishe tafiti kutokana na mvutano usio na maslahi kwa nchi,” alisema.

Lowassa atoa kauli

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge Edward Lowassa, alisema jana kuwa kamati yake imesikia suala hilo kwenye vyombo vya habari na inajipanga kuzifanyia kazi taarifa hizo mara moja.

"Tumesikia kupitia vyombo vya habari na kama kamati tutahakikisha tunazifanyia kazi," alisema Lowassa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano aliouitisha kuzungumzia safari ya kamati yake nje ya nchi.

Chadema yatoa tamko
Kwa upande wake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeonya kuwa tatizo la ufisadi halitaisha nchini hadi pale Serikali itakapochukua hatua za dhati za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wote ambao wamehusika na ufisadi wa raslimali za nchi.

Chama hicho kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuagiza kukamatwa kwa watuhumiwa wote wa ufisadi wa ununuzi wa rada na wale ambao wanatuhumiwa kuhifadhi Sh 303.7 bilioni nchini Uswisi.

“Chadema kinatambua kwamba kuachwa kwa mafisadi bila kuchukuliwa hatua kamili za kisheria na mali zao kufilisiwa, kunafanya taifa kuendelea na ufisadi ikiwemo ule wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Richmond na sasa tuhuma mpya za ufisadi wa shilingi bilioni 303 kwenye akaunti Uswisi,” ilisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, kupitia taarifa kwa 
vyombo vya habari jana. 
Wizi mwingie kupitia mtandao

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Ame Silima alilieleza Bunge jana kuwa hadi sasa kiasi kilichoripotiwa Polisi kuhusina na wizi kwa njia ya mtandao nchini ni Sh2.2 bilioni.
Fedha hizo ni zimegawanywa katika makundi matatu, Sh1.3 bilioni, Euro 8,897 (Sh17,660, 545) na dola 551,777 (Sh882,843,200).

Kauli hiyo ilitolewa wakati Waziri Silima akijibu swali la Hussein Mussa Mzee (Jang’ombe-CCM) aliyetaka kujua ni kiasi gani cha fedha kimeripotiwa Polisi kutokana na wizi kwa njia ya mtandao.
Mzee alihoji Serikali imejipanga vipi kudhibiti wizi wa mtandao, idadi ya waharifu wa wizi huo ambao wamekamatwa huku akitaka itungwe sheria maalumu kushughulikia wizi huo.
Silima alisema kuwa Serikali imetunga sheria inayoshughulikia uhalifu unaofanywa kwa njia ya mtandao, Electronic and Posta Communication Act, 2010 na sheria ya kudhibiti fedha haramu (The Anti – Money Laundering Act – 2006.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia vyombo mbalimbali vya dola kama vile Polisi, taasisi za fedha, vyombo vya habari, TRA na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imejiwekea mikakati ya kuelimisha wananchi kuhusu aina ya uharifu wa kimtandao na jinsi ya kupambana nao.
Waziri alibainisha kuwa jeshi la Polisi limeanzisha Kitengo cha Makosa ya Kimtandao (Cyber Crime Unit) ambacho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kinafanya kazi kubwa ya kupambana na majanga hayo.
Kilio cha wabunge

Wakati huohuo wabunge wameendelea kumbana Pinda huku baadhi yao wakikataa kuunga mkono hotuba yake hadi pale atakapojibu hoja walizotoa.
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy akichangia hotuba ya hiyo jana, alisema vita dhidi ya ufisadi haiwezi kufanikiwa kwani vyombo vya husika wakiwamo Takukuru wanashindwa kuchukua hatua kwa makosa ambayo yako wazi.
 
Keissy alisema mafisadi na walarushwa nchini wanalindwa na Takukuru, kwani licha ya kuwapo kwa ushahidi na viashiria vya wazi, chombo hicho hakichukui hatua zozote.
 
Alisema, kama wapo watu wanaodiriki kuuza dawa ambazo zilipaswa kupelekwa katika hospitali na matokeo yake wagonjwa wanakufa, mtu huyo hana budi kunyongwa.
 
“Sheria za nchi hii zinawalinda wezi, ndiyo maana ufisadi hauwezi kuisha, mtu ana majengo makubwa leo, wakati ni jana tu amepata ubunge, amepata wapi utajiri huo wa haraka, aulizwe na akishindwa kutoa maelezo achukuliwe hatua,” alisema Keissy na kuongeza:
 
“Sasa la ajabu ni kwamba eti wanakwambia kwamba kama unamjua mla rushwa basi uwapelekee taarifa, kwani wao hawawaoni watu wanaotajirika haraka haraka?” alihoji.
 
Keissy ambaye aliipinga Bajeti ya Waziri Mkuu hadi pale atakapopewa majibu ya kuridhisha, alisema sheria za nchi hii ni dhaifu, ndiyo maana mafisadi wanaoiba mamilioni wanaendelea kudunda barabarani wakati mwizi anayeiba simu hupigwa na kuchomwa moto hadi kufa.
 
Mbunge huyo alisisitiza ujumbe wake, akisema kuwa, “hata ikitokea mafisadi hao wakafariki basi pingu ziwekwe juu ya makaburini yao.”
 
Naye Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Riziki Lulida alisema kuna njama zinazofanyika za kudhoofisha maendeleo mkoani Lindi kwa kuwapeleka viongozi wala rushwa katika mkoa huo.
 
Alisema, uduni wa mkoa huo unasababisha wapinzani kuufanya kuwa kichaka cha wapinzani, kuwadhalilisha na kuwasema kwamba wao ni maskini.
 
“Viongozi wengi wa halmashauri wanaofanya ubadhirifu wa fedha kutoka mikoa mingine hutupwa Lindi,” alisema Lulida kabla ya kuanza kuwataja kwa majina wafanyakazi hao wa halmashauri:
 
“Joachim Materu ameiba 577 milioni, akapelekwa Lindi, Eunice Maro ameiba 262 milioni na akapelekwa Lindi, baada ya kufanya wizi huo, Maro aliziweka katika akaunti inayoshukiwa kuwa ni ya rafiki yake, yenye akaunti namba 206660017 NMB ambaye alihamishiwa Ofisi ya Kilimo Lindi,” alisema.
 
Aliwataja wengine kuwa ni Macha anayetuhumiwa kuiba Sh6 bilioni ambaye amehamishiwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na kwamba kuhamishwa kwao ni kusambaza ufisadi katika maeneo mengine.
 
Lulida aliongeza kuwa, kama Waziri Mkuu anataka aiunge mkono bajeti yake, basi aje na majibu sahihi kuhusu maendeleo mkoani Lindi pamoja na kurudisha programu ya kilimo ya Kanda ya Kusini, (SAGCOT)

Habari hii imeandaliwa na Neville Meena, Florence Majani na Habel Chidawali, Dodoma na Leone Bahati Dar

11:09 PM | Posted in | Read More »

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added