Ukweli Kuhusu Ugomvi Wa Mapacha Watatu huu Hapa
Repa Khaleed Chokoraa kutoka band ya Mapacha Watatu amekanusha stori kwamba ugomvi uliotokea kwenye band hiyo uliwahusisha Josee Mara na Kalala Junior na kupigana. Amesema “Kalala hajapigana wala kugombana na Josee nashangaa magazeti yameandika hivyo, Kalala alihitilafiana kiswahili na mpiga gitaa wetu Allan Kiso” “Chanzo cha ugomvi wao ni pale ambapo Kiso alitaka kumkatisha Kalala kuimba kwa kutumia gitaa wakati wakiwa kazini, hiyo yote ilikua ni ishara ya Kiso kutaka kalala aache kuimba kutokana na maneno ambayo alikua anayatoa Kalala kwenye mic sasa hicho kitendo Kalala hakukipenda ambapo show ilipoisha ndio wakalumbana tukaawaamu yakaisha” – Chokoraa Chokoraa amethibitisha kwamba toka ugomvi utokee mpaka sasa Kalala hajaja kazini na wamejaribu kumuita kwenye vikao mara mbili ili waweke mambo sawa lakini hajatokea, bado millardayo.com inaendelea kumtafuta.