|

Torres Asema kukaa Benchi Sio Issue

 Mchezaji wa Chelsea Fernando Torres jana ameifungia timu yake ya taifa ya Hispania magoli mawili kwenye mechi na Ireland ndani ya mzigo wa Euro 2012.

Torres amesisitiza kwamba hana noma kama kocha wa timu ya taifa atamuweka benchi kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Croatia, anasema yeyote anaweza kucheza kwa sababu kikosi kina wachezaji wakali kwa hiyo kukaa benchi sio ishu.
Torres alichezeshwa dakika chache sana kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Italy ila jana kocha alimpa muda wa kutosha ambapo alionyesha ujazo wake kwa kulifungia taifa lake magoli mawili kwenye hiyo mechi ambayo walishinda nne bila ushindi ambao umeiweka Hispania kileleni kwa kufuzu kuingia kwenye mtoano.

Posted by Unknown on 6:27 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added