|

Alichosema AT kuhusu Wimbo Mpya wa Offside Trick

 Tunafahamu kwamba AT ana beef na kundi la OFFSIDE TRICK ambalo siku kadhaa zilizopita member wake Muda alitangaza kujitoa ili kupumzika kufanya muziki hivyo nafasi yake ikachukuliwa na Hammer Q.

Offside Trick linalounda na Lil Gheto na Hammer Q tayari limeanza kupiga mzigo.

Japo bado hawajapatanishwa wala kuzungumza toka ugomvi uanze, AT amekubali kuizungumzia picha aliyonayo kuhusu kundi hilo kwa sasa.

Kuhusu muunganiko wa Lil Gheto na Hammer Q amesema “labda wao wenyewe wanahisi  combination yao iko sawa hata mimi naona nyimbo wanazotengeneza sio mbaya japo wote tuko kwenye ushindani wa muziki, wimbo wao mpya wa babu jinga ni mzuri wamejitahidi wameimba vizuri Mungu awazidishie”

Amesema “sijaushika huo wimbo lakini naipenda hasa ile sehemu  mwanzoni Mudacris anasema muziki wetu ule ule na unakwenda level ya kimataifa, beat yake ni nzuri huo wimbo na uko kwenye cd yangu nyumbani kwa sababu msanii mzuri ili uendelee kuwa mzuri ni lazima usikilize nyimbo za wenzako hata kama kuna ubaya wowote nitaendelea kusikiliza wimbo wa mtu yeyote kwa sababu nataka kuwa msanii mzuri, na watanzania walishanikataza kuhusu kugombana hivyo sitaki kupoteza bahati niliyonayo alafu watu wakaanza tena kunichukia”


Posted by Unknown on 6:23 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added