|

'TFF wameniondoa Twiga Stars'


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Wanawake (Twiga Stars), Charles Mkwasa amelitupia lawama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kusema ndiyo kiini cha yeye kuachia ngazi kuifundisha timu hiyo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Mkwasa alikariri na baadhi ya vyombo vya habari akitangaza kuachia ngazi ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa na Ethiopia na hivyo kukosa fursa ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baadaye mwaka huu.

Akiongea na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, Mkwasa aliyeiwezesha Stars kucheza Fainali za Afrika mwaka jana nchini Afrika Kusini, alisema uamuzi wake ni kutokana na kutothaminiwa na TFF.Mkwasa alisema hakuna mtu aliyemshawishi kufikia uamuzi huo, bali ni ridhaa yake binafsi kama sehemu ya kuwajibika kwa faida ya soka la Tanzania.

"Ni kweli mimi siyo tena kocha wa Twiga, nimeamua kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa wengine kuendelea, nilipofika inatosha kabisa," alisema Mkwasa.

"Nimekuwa na timu kwa muda mrefu na nimefanya mengi pia, nadhani sasa nitoe nafasi kwa wengine waendeleze mazuri niliyofanya," aliongeza Mkwasa.Alisema anatarajia kukabidhi barua yake kujizulu kwa waajiri wake TFF wakati wowote kuanzia sasa.

Posted by Unknown on 1:54 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added