|

Sikiliza Alichosema Dully Sykes Baada ya Kutoa Matusi Redioni..

Juzi kwenye show ya XXL Clouds fm msanii Dully Sykes alisababisha lawama nyingi zimpate kutoka kwa fans wake na watu wengine baada ya kutoa tusi kwa Gossip Cop Soudy Brown anaefanya  YOU HEARD.
Ni kuhusu new single ya Mwana Fa ft Ay na Dully Sykes – Ameen ambayo imetengenezwa na Dully ambapo baada ya kuachiwa Soudy Brown aligundua kwamba ni kama inafanana na single ya staa wa Jamaica.
Baada ya hapo Soudy ilibidi ampigie Mwana Fa ambae alimjibu vizuri tu kwamba kweli ile single imefanyiwa sample lakini akamuelekeza Soudy Brown aongee na Dully kwa sababu yeye ndio producer na ndio mtu sahihi wa kuliongelea hilo.
Soudy alipompigia Dully hakufanikiwa kupata lolote zuri bali aliambuliwa kujibiwa kwa mkato na mwisho Dully Sykes akamwambia siongei na mashoga na hiyo ilikua ni baada ya staa huyo mkazi wa Tabata Dar es salaam kumuuliza Soudy kama amekosa kazi ya kufanya.
Usiku wake baada ya watu kuzidi kutuma msg on air kwamba wamechukizwa na tusi alilotoa Dully, Dully alinipigia simu akaomba tukutane Kinondoni baada ya mimi kumaliza AMPLIFAYA saa 3 usiku, nimewahi kufanya interview na Dully Sykes mara nyingi tu ila kiukweli sijawahi kumuona Dully akiwa amenyongo’nyea na kuumia kiasi kile.
Nilipoanza kumrekodi alisema “kweli nimekosea ni kwa sababu hakunikuta kwenye mood, naomba msamaha wanisamehe mashabiki na kwenye Media pia, wanisamehe kwa kile ambacho nimeongea ilikua ni hasira tu wasikilizaji wote ambao wamesikiliza na mashabiki zangu wote wasinielewe vibaya, nilikua na hasira nilikua na mambo yangu mwenyewe kichwani”
Isikilize YOU HEARD ambayo Dully Sykes alitukana, chini yake ndio kuna sauti ya Dully Sykes akiomba msamaha.

Posted by Unknown on 4:03 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added