Nyumba ya Wema Yaleta Utata, Yadaiwa si Yake
ILIANZA
chinichini kuwa fedha imemtembelea Wema Isaac Sepetu akithibitisha
kumiliki nyumba ambayo ndani yake ina mazagazaga yanayoifanya kuwa na
thamani ya Sh. milioni 400 lakini nyuma ya stori hiyo kuna zengwe, shuka
na Ijumaa upate ‘udambwidambwi’ kamili.
KIJITONYAMA, DAR
Kwa
mujibu wa chanzo kisicho na shaka ambacho ni mmoja wa mashosti wa Wema,
nyumba hiyo anayotarajia kuhamia hivi karibuni ipo Mtaa wa Bwawani,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
MADAI MABICHI
Kikifichua
mambo mazito nyuma ya pazia, chanzo hicho kilidai kuwa watu wanaoijua
ishu hiyo kiundani walipigwa na butwaa waliposikia Wema anamiliki mjengo
huo wa kifahari huku wao wakielewa vingine.
“Ninavyojua ile nyumba siyo yake bali amepanga tu,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Aisee!
Nimeshangaa kusikia Wema kanunua lile jumba wakati mchakato wa kwanza
wakiwa na madalali walikuwa wakitafuta nyumba ya kupanga.
“Kusema
kweli jambo lililonishangaza ni kuwa mpaka mchakato wa mwisho
unafanyika kuhusiana na nyumba hiyo ni kwamba Wema alikuwa anaipangisha
na siyo kuinunua.”
SIKIA HILI JIPYAAA
Wakati
tukisikiasikia hayo, tukaletewa lingine jipya na sosi mwingine kuwa
Wema alipewa jumba hilo lililokuwa likimilikiwa na mama Ngoma ili
amalizie kurekodi filamu yake mpya ya The Superstar.
“Si
mnakumbuka alivyofanya juzikati kwa kuvishwa pete ya uchumba na Mwinyi
wa Machozi kumbe alikuwa anarekodi filamu, ndiyo hivyohivyo kwa hili
jumba, kama hamuamini mtaona baadaye.
“Wewe
angali vizuri hizo picha, ni za filamu kabisa kwani kipande cha hiyo
muvi kinamtaka aonekane akiishi maisha ya kistaa sana. Wewe nyumba gani
umetenga mpaka chumba cha kuzungumza na vyombo vya habari?” alihoji sosi
huyo.
UTATA
Wakati
mambo yakizidi kuwa mengi, kikaibuka chanzo kingine kikidai kuwa si
kweli kwamba mjengo huo unamilikiwa na mama Ngoma bali ni ya Mwarabu
fulani.
Baada ya kuambiwa vitu kibao kuhusu jumba hilo, Ijumaa lilianza kusaka ukweli ili kujibu maswali ya mashabiki wa Wema.
HUYU HAPA MENEJA WAKE
Mtu
wa kwanza kuzungumza na Ijumaa ni meneja wa Wema, Martin Kadinda ambaye
alikiri Wema kununua nyumba hiyo lakini si kwa Sh. milioni 400.
“Unajua huyo anayesema kuwa Wema amepanga siyo kwamba anakosea ila anachelewa kujua mambo.
“Ni
kweli kabisa mara ya kwanza Wema alikuwa anataka kupanga nyumba hiyo
lakini baadaye alikaa chini na mwenye nyumba na kukubaliana kufanya
biashara ya kumuuzia lakini si kwa Sh. milioni 400,” alisema Martin.
MILIONI 400 KIVIPI?
Akifafanua fedha hizo zinazodaiwa kununulia mjengo huo, Martin alisema:
“Hiyo milioni 400 ni thamani ya nyumba na vitu vyote vya ndani. Siyo bei iliyonunuliwa.”
PEDESHEE WEMA LAIVU
Ieleweke kuwa siyo kwamba hatumuamini Martin lakini tulizungumza na Wema ili mashabiki wake wamsikie mwenyewe.
Katika mahojiano maalum na Ijumaa, Wema alikiri kuwa anamiliki nyumba hiyo.
“Ni kweli namiliki nyumba hiyo ambayo ina thamani ya milioni 400, hao wanaosema nimepanga watajiju.
“Siwezi
kununua fenicha za mamilioni ya shilingi halafu nishindwe kununua
nyumba,” alisema Wema ambaye leo atakuwa jaji wa Shindano la Miss Dar
City Center 2012 kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Masaki jijini Dar.
ANAPATA WAPI FEDHA?
Katika
siku za usoni, Wema maarufu kwa jina la Pedeshee Mwanamke anapokuwa
ukumbini kufuatia tabia ya kuwamwagia ‘mihela’ wanamuziki, amekuwa
akifanya mambo makubwa yanayogharimu mshiko mrefu hivyo kuibua maswali
mtaani.
Mfano,
miezi kadhaa iliyopita alikwenda Dubai kufanya ‘shoping’ ya zaidi ya
Sh. milioni 60, hajakaa vizuri akavuta mkoko mwingine tofauti ile Toyota
Lexus Harrier unaoitwa Toyota Mark X huku akikamilisha filamu yake
iliyogharimu Sh. milioni 68 kuitengeneza.
Weka hayo yote pembeni, anatarajia kufanya uzinduzi wa kampuni lake la filamu ambalo kila kitu kimekamilika.
Kufuatia kufuru hizo na nyingine ambazo hazijaorodheshwa hapo juu ndiyo maana kukaibuka maswali kuwa anapata wapi jeuri hiyo?
TUMALIZIE NA HAYA MADAI
Madai
ambayo huwa Wema hataki yaguswe ni kuwa eti ana mwanaume mwenye fedha
zake aliyempata baada ya kuachana na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Eti
wanasema ndiye anayempa jeuri yote hiyo huku nyuma kukiwa na madai kuwa
ni jamaa anayefanya kazi idara nyeti serikalini (tunalifanyia kazi
tupeni muda kiduchu)