|

Drogba sasa huenda akatua Barca



DIDIER Drogba anaweza kufanya uhamisho wa kushangaza kuhamia Barcelona ya Hispania ikiwa ni muda mfupi tangu kusaini mkataba wa kuichezea timu ya  Shangha Shenhua ya China.
Nyota huyo wa Ivory Coast, aliachana na klabu yake ya Chelsea aliyoiwezesha kutwaa taji la Klabu Bingwa Ulaya na kuamua kwenda China.
Alitarajia kwenda mjini Barcelona kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Wakurugenzi wa klabu hiyo. Mazungumzo hayo yalipangwa kufanyika Jumanne wiki hii.
Drogba (34) alitarajia kulipwa mshahara wa pauni 200,000 (Sh483 Milioni) kwa wiki na klabu hiyo ya China.
Aliposaini alisema: "Nathibitisha nimesaini kucheza klabu ya Shanghai Shenhua ya China kwa miaka miwili na nusu. Nitarejea kujiunga na klabu Julai.
"Nimetafakari ofa zote nilizopewa wiki kadhaa zilizopita, lakini nadhani Shanghai Shenhua ni sehemu sahihi kwangu kwenda kwa muda huu.
"Najiandaa kukutana na changamoto mpya na kujifunza utamaduni mpya pia. Lakini pia nafurahia kusikia maendeleo ya Ligi Kuu China.
"Chelsea ilipokwenda China mwaka jana, tulikuwa na fursa nzuri na mashabiki walitufurahia. Natarajia kuitangaza ligi ya China duniani kote," alisema Drogba.

Posted by Unknown on 11:16 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added