|

Mhh ! Mwigizaji Zamda Salimu Kwa Pombe ni Noma


MUIGIZAJI mwenye vituko vingi pindi awapo sehemu ya starehe, Zamda Salim ‘Zam Minaj’ juzi kati alionekana kituko baada ya kupiga ‘mitungi’ kwa wingi iliyosababisha aonekane kituko mbele za watu.
Tukio hilo la kupiga ‘maji’ mithili ya mamba lilichukua nafasi katika Ukumbi wa New Maisha Club uliopo Masaki jijini Dar, ambapo muigizaji huyo alifika pande hizo kwa ajili ya kula bata.
Mishale ya saa 7:00 usiku, msanii huyo alionekana akiwa amesizi kwenye meza ya pekee huku akiwa bwii, mwandishi wetu alipomsogelea na kutaka kumfotoa picha aligeuka mboga huku akisema kilevilevi:
“Jamani nini, mboni hivyo hata huku mnatufuata acheni hizo bwanaaa…mnatuharibia raha zetu.”
Hata hivyo, baada ya muda msanii huyo aliyewahi kuapa kuwa hatakunywa tena pombe alionekana akitoka ukumbini hapo akiwa na mashosti zake kisha kutokomea kusikojulikana.

Posted by Unknown on 12:03 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added