12:22 AM | Posted by Unknown
Mlipuko wa bomu la juzi Nairobi Kenya ulipotokea, swali la kwanza ambalo wengi waliuliza baada ya kupata taarifa, lilikua ni wamepoteza maisha watu wangapi? Taarifa kamili ilipotoka baadae ikaonyesha hakikutokea kifo chochote ila majeruhi walikua zaidi ya 25, wengine walitibiwa na watano wakabaki hospitali kutibiwa manake walikua katika hali mbaya.
Taarifa za leo kutoka Nairobi ni kwamba mmoja wa hao waliokua wamebaki hospitali aitwae LESIYAMPE amefariki dunia alfajiri ya May 31, Afisa mkuu wa hospitali ya Kenyata amethibitisha.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Polisi wa Kenya wamethibitisha kumkamata mtu anaedaiwa kuhusika kulipua bomu hilo juzi, alikamatwa akiwa kwenye uwanja wa ndege Nairobi akijiandaa kwenda Congo DRC.
Posted by Unknown
on 12:22 AM. Filed under
feature,
Nje
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0.
Feel free to leave a response