|

Wema na JB wazua Jambo Zanzibar


Na Imelda Mtema
MASTAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Jacob Steven ‘JB’ hivi karibuni walizua jambo walipokuwa Zanzibar kufuatia mapozi tata waliyokuwa wakijiachia nayo mbele za watu.
JB na Wema ambao walikuwa miongoni mwa wasanii waliokwenda kumpa ‘tafu’ mwenzao, Issa Musa ‘Claud’ kwenye uzinduzi wa filamu yake ya Toba uliofanyika ndani ya Hoteli ya Bwawani, walionekana wamegandana kiasi cha baadhi ya watu kudhani ni Mr na Mrs.
Awali, wawili hao walizama hotelini hapo huku JB akiwa amemuweka ‘kwapani’ Wema lakini hata walipoingia ndani, walikaa pamoja.
Aidha, tukio lililozidisha minong’ono ni lile la Wema kuegamia mabegani mwa JB kisha kuuchapa
ambapo mmoja wa watu waliokuwepo ukumbuni hapo alisikika akisema: “Mh...wana mambo hawa, atawezaje kumlalia mwanaume ambaye siyo wake hadi kulala vilee?”

Posted by Unknown on 12:00 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added