KWA NINI JOHN MNYIKA AMESIKITISHWA NA KAULI ZA WAZIRI MPYA WA FEDHA.
Baada ya kushinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomfanya kuwa mbunge wa Ubungo kupitia Chadema, John Mnyika ameibua jingine kwa kusema anazo nyaraka za ndani ya benki kuu kuhusu kinachoendelea juu ya matumizi ya serikali.
Amesema “nitakwenda kuongeza nguvu za kibunge kuhakikisha uwajibikaji kwenye maswala haya ya msingi ambayo yanawagusa wananchi, na kwakuwa nilishaanza huko nyuma kutoa kauli kuhusu maswala haya ya mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha na waziri wa wakati huo bwana Mkulo akaahidi akatoa kauli ya kunijibu kwa kusema tayari alipeleka kwenye baraza la mawaziri kuhusu mpango wa kudhibiti hili jambo lakini nimesikitishwa na kauli za Waziri mpya, hazitii matumaini katika ushughulikiaji wa mfumuko wa bei na matatizo ya kupanda kwa gharama za maisha”
Hiyo ndio kauli ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika ambae alishinda kesi Alhamisi May 24 2012 na kusema kwamba “hiyo kesi haikua na madai ya msingi, imepoteza muda wetu wa kazi na imeingiza gharama pamoja na kwamba tutazidai lakini kuna gharama ambazo kodi za wananchi zimetumika Mahakamani za kuendesha hii kesi, ni lazima tubadili mifumo yetu ya kikatiba na kisheria ili kutoliingiza taifa kwenye hasara ya madai yasiyokua ya msingi”