|

AY akamilisha shooting ya video yake Afrika Kusini, kufanya nyingine mwezi ujao!


Kazi ya kushoot video ya Ambwene Yesaya aka AY iliyofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini imemalizika salama jana.
AY aliambatana na producer wa wimbo huo uliokuwa ukifanyiwa video, Marco Chali wa Mj Records.
Video hiyo ambayo kwa mujibu wa AY imegharimu $20,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 30 za Tanzania, imeongozwa na director wa Nigeria anayeishi nchini Afrika Kusini Mike Ogeke wa kampuni ya GodFather Productions.
Wakati wa shooting hiyo wanamuziki mapacha wa kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye walikuwepo japo haijulikani kama wataonekana kwenye video ya AY kwakuwa nao walikuwa wakifanya video yao na kampuni hiyo.
Baada ya kukamilisha shughuli hiyo AY alitweet,” I_Am_Godfather are very professional,great team EVER,we gonna shoot more videos with them.”
“Had a great shoot with Tanzanian hottest artist, @AyTanzania! #its a wrap! Good working with you sir!” aliandika mmoja wa watu waliohusika kushoot video hiyo.
Katika hatua nyingine AY amesema kuwa ana mpango wa kufanya video nyingine na kampuni hiyo mwezi ujao, “I am going to shoot another one around June.”

Posted by Unknown on 4:41 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added