D’Banj awa rais wa Def Jam Africa
Mwanamuziki wa Nigeria D’Banj aka Koko Master anasemekana kuwa sasa ndiye rais wa Def Jam Africa.
Muimbaji huyo wa Oliver Twist anasemekana kuwa muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo mnono naye fasta amemsainisha msanii anayechipukia Davido kwenye record label hiyo.
Davido ataungana na ndugu yake D'Banj K-Switch kwenye label ya Def Jam Africa. Hata hivyo haijafahamika ni vipi msanii huyo atajigawa na deal ya Mercury Records ya Uingereza na G.O.O.D Music aliyopo chini yake.
Katika hali inayoonesha mambo kuendelea kumnyookea msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Dapo Oyebanjo, jumapili hii pia aliweka historia nyingine baada ya remix ya wimbo wake Oliver Twist kukamata nafasi ya tisa katika chart ya Uingereza.
Def Jam Records inayomilikuwa na Universal Music Group, na kufanya kazi kama sehemu ya The Island Def Jam Music Group ni record label ya Marekani ambayo imejikita katika muziki hip hop na muziki wa mjini.
Wakati wa uongozi wa Jay Z, Def Jam ilifanikisha kuwatoa wasanii kama Rihanna, Ne-Yo, na Kanye West.