Alichosema Will Smith kuhusu Mwanaume alietaka kumbusu
Hivi ndivyo ilivyokua wakati mwandishi huyo alipotaka kumbusu Will Smith. |
Mwigizaji Will Smith
amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kumsukuma mwandishi wa habari
wa kiume alietaka kumbusu kwenye Red Carpet huko Moscow wakati
mwigizaji huyo alipokwenda kuitambulisha movie yake mpya ya MEN IN BLACK
3.
Mwandishi huyo alifika na
kumwambia Will Smith kwamba yeye ni shabiki yake mkubwa hivyo akaomba
kumkumbatia na baadae akataka kumpiga busu ndipo Will Smith
alipokasirika na kumsukuma kwa hasira.
Alichosema Will Smith ni kwamba
waandishi wenzake na huyo jamaa walimuomba msamaha na kusema kwamba
jamaa huwa ni mchekeshaji labda alifanya hivyo kwa nia ya kuchekesha na
hakua na maana mbaya.