Alichosema Nazizi kuhusu wanao mponda Prezzo kwenda Big Brother
Baada ya Prezzo kuwa topic
kubwa kwenye mitandao ya kijamii ya twitter na facebook hasa kwa baadhi
ya wakenya ambao wamekua wakiponda yeye kwenda big brother akiwemo
msanii Jaguar, mshkaji wa karibu wa Prezzo, mkali Naziz wa Necessary
noise amekubali kuelezea wengi wasichofahamu kuhusu Prezzo.
Amesema “sijaangalia Big
Brother lakini nimekua nikiona watu wanamuongelea kwenye twitter na
facebook, lakini kuna sababu zilizofanya watu waliokwenda Big Brother
kuchaguliwa, lazima walijua Prezzo ni mbishi ni mtu ambae ni sahihi
akiwepo sehemu kama hiyo”
kwenye sentensi nyingine Naziz
kasema “Prezzo ni mbishi ni rafiki yangu namjua japo sijaangalia Big
Brother najua lazima ubishi utakuepo na huwa hasikilizi na uhakika
kwamba wasichana watakua wanamchukia kinoma au watakua wanampenda,
vilevile ni Mkenya na inabidi tumsupport”
Kwa kumalizia Naziz amesema
“watu wanamchukulia yule Prezzo kwa Big Brother kwa kile wanachokisoma
kwenye Media kuhusu yeye lakini Media na Prezzo hawajawa kwenye uhusiano
mzuri, yani hata kama Prezzo anajaribu kufanya nini Media Kenya bado
ilikua inamdiss wakati wote kwa sababu ni CMB na anajiona ana pesa
lakini ni mtu tofauti wakimpa nafasi watamjua vizuri, sitazami Bog
Brother lakini namuunga mkono”
Hiyo ni kauli ya Naaziz ambae
sasa hivi yuko Bongo kwa ajili ya kuperform leo Zonghua Garden Dar es
salaam kwenye Reggae show ambayo itakua na vichwa vikali vingine kama
washindi wa KTMA 2012, Warriors from the East pamoja na 20%.
Mpaka sasa Naaziz ni mmoja kati
ya wakenya wachache walioperfom Tanzania mara nyingi, alianza kuperform
bongo miaka 15 iliyopita.