|

Hussein Machozi akana kuwa na uhusiano na Avril (Kenya)


Hussein Machozi
Kuna story zinavuma nchini Kenya kuwa Mzee wa ‘Kafia Ghetto’ na ‘Full Shangwe” Hussein Machozi ana uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wanamuziki warembo kabisa Afrika Mashariki, Avril Nyambura!

Hata hivyo Hussein mwenyewe amekataa kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Wawili hao wamedaiwa kuwa na uhusiano baada ya kuonekana mjini Mombasa wakiwa karibu mno baada ya show waliyokuwa pamoja.

 “Avril ni rafiki yangu wa karibu kama msanii yeyote yule. Mimi niko single na muda wa mambo hayo utafika tu” Hussein ameiambia website ya The Star ya nchini Kenya.

Avril
Baada ya kusoma taarifa hiyo tumemuuliza pia Hussein kuhusiana na tetesi hizo ambaye amejibu "aaah hamna bana labda wameona tupo karibu tu wakaona namgonga bana..wala hakuna kitu na huyu mtoto.."

Katika hatua nyingine Machozi amerekodi wimbo uitwao 'Addicted' na mwanadada anayetamba sana kwa sasa nchini Kenya Size 8. Machozi anasema wimbo huo ni kwaajili ya mashabiki wake wa kike ambapo video ya wimbo huo itafanywa na kampuni ya Ogopa DJs ambao ndio walioutengeza wimbo huo.

Posted by Bongo Flavor on 10:18 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added