|

Bongo Movies News: Husna Idd (Sajenti) Asusiwa Siku ya Birthday yake


MWANADADA anayeuza nyago kwenye filamu Bongo, Husna Iddi ‘Sajenti’ amedaiwa kususiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa ‘bethdei’ na wasanii wenzake wa Bongo Movie iliyofanyika nyumbani kwao, Sinza jijini Dar.
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitutonya kuwa, katika sherehe hiyo Sajenti alitarajia kupata kampani kubwa kutoka kwa wasanii wenzake hao lakini ikawa tofauti na matarajio yake.
“Alifanya sherehe pale nyumbani kwao na alitarajia wasanii wa Bongo Movie kuhudhuria lakini hakuonekana hata mmoja hali iliyosababisha pati idorore,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kujua sababu za msanii huyo kususiwa sherehe yake, mwandishi wetu alimtafuta Sajenti na alipopatikana alisema:
“Kweli nilifanya ‘bethdei’ na siyo mimi niliyeandaa, niliandaliwa na marafiki zangu wengine akiwemo Jack wa Maisha Plus na sikuwa na taarifa kwani walinifanyia sapraizi, hivyo siyo kweli kuwa wasanii wenzangu walinisusia. Yaani mimi Husna nisusiwe? Hiyo haitatokea.”

Posted by Unknown on 12:09 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added