|

Eryne Epidu adai Mike Tee ndiye alimtimua Bongo


Video Producer wa zamani wa Showbiz defined inayomilikiwa na Msanii Mike Tee, Eryne Epidu, ameweka wazi kisa cha bifu yake na patner wake huyo wa zamani kwenye kampuni hiyo ambayo Eryne anadai waliianzisha pamoja wakiwa yeye, Mike Tee na msanii Witness.

Eryne ameelezea kwa uchungu jinsi Mike Tee alipomfanyia visa baada ya wao kuachana kikampuni na yeye kufungua kampuni yake mwenyewe ya inayojulikana kama Blaze Video. Amesema kwamba sababu yake kuu ya kuachana na Showbiz defined ilikua ni madeni mengi yaliyolimbikizwa na Mike Tee na kwamba kilimuuma sana yeye Eryne alivyondoka na kuamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe.
Eryne amesema Mike Tee alimlengesha kwa maofisa kwa uhamiaji na kupelekea kumtimua nchini na kurudi kwao Uganda.
‘Nliiona Bongo chungu ghafla baada ya Mike Tee kunitumia maofisa uhamiaji ndio maana nimeamua kuondoka Dar na kuja kupumzika Uganda kwetu. sijui kama ntarudi Bongo ila ningependa kwanza kujipanga ili hata kama ipo siku ntarudi, nitakuja kikamilifu kupiga mzigo kama kawa,’alisema Eryne.
Mike Tee alieleza waliachana kiofisi na kila mtu aliamua kutafuta maslahi kivyake na alikanusha kumtimua Eryne nchini.

Posted by Bongo Flavor on 1:24 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added