|

Diamond achafuka ukweni-Click kusoma zaidi

Na Shakoor Jongo
ILE skendo ya kunaswa hotelini na mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel bado inamtesa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambapo safari hii anadaiwa kuchafuka vibaya upande wa wakwe zake kwa mchumba’ke Jokate Mwegelo, Ijumaa linafunguka.
Habari kutoka kwenye chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao zinadai kuwa baada ya habari hiyo kubumburuliwa na gazeti damu moja na hili, Risasi Jumamosi ndiyo iliyotibua mambo ukweni kwake hivyo kuonekana siyo.
MSURURU WA WANAWAKE
Ilidaiwa kuwa habari hiyo ndiyo iliyotonesha kidonda kilichokuwa kinataka kukauka cha ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva kutajwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake mastaa na wasiokuwa mastaa.
“Asikwambie mtu, unajua upande wa akina Jokate ni watu wa dini sana. Yaani kwa skendo skendo kama hizo, wanamuona Diamond kama anataka kuwachafua.
“Unajua zile ishu za kudaiwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake zilikuwa zimeanza kutulia kwa sababu yupo na Jokate lakini baada ya kutokea hii ya kunaswa hotelini na Aunt, imetibua mambo kule ukweni na mbaya zaidi anaonekana hajatulia,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
HUYU HAPA DIAMOND
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa lilimvaa Diamond kavukavu ambapo katika kuthibitisha kuwa vyanzo vyetu vya habari havibahatishi, alikiri kuchafuka ukweni huku akiongeza kuwa anahisi kuna watu nyuma ya habari hizo ambao wamelenga kumharibia mambo yake.
“Naomba niweke wazi jambo hili kwa sababu ni kweli nachafuliwa.
“Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate, nahisi wanaweza kufanikiwa,” alisema Diamond Platnumz.
UHUSIANO WAKE NA JOKATE
Kufuatia ishu hizo, uhusiano wa kimapenzi wa kidume huyo na mwanamitindo Jokate unadaiwa kuwa kwenye hatihati pamoja na kwamba bado wapo pamoja.
TULIKOTOKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond na Aunt walidaiwa kubambwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, Dar wakila ‘good time’, hivyo kuzua tafrani kwenye uchumba wa mwanamuzi huyo na Jokate.
Mbali na madai hayo yanayomhusisha Diamond na Aunt ‘kuminya’ pamoja, kichwa hicho cha Bongo Fleva kiliwahi pia kutajwa kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper, wauza nyago kwenye video za muziki, Rehema Fabian na Natasha, staa wa Maisha Plus, Pendo Moshi kabla ya kumchumbia Wema Sepetu kisha wakamwagana na kujikuta mikononi mwa Jokate.

Posted by Unknown on 11:16 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added