|

Mdogo wa Kanumba Seth Afunguka kuhusu penzi la Kanumba na Lulu


Erick Evarist na Gladness Mallya
KWA mara ya kwanza, mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco ameufungukia uhusiano wa kimapenzi uliokuwepo kati ya kaka yake na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ akieleza kuwa, haukuwa na malengo ya baadaye.
Akizungumza na waandishi wetu juzikati kwenye ofisi za Kanumba The Great Film, zilizopo Sinza jijini Dar, Seth alisema penzi la wawili hao halikuonekana kuwa la kudumu kama baadhi ya watu wanavyodhani kwani marehemu hakuwahi kuzungumzia matarajio yake na binti huyo.
“Sitaki kuamini kuwa wawili hao walikuwa na mapenzi endelevu kwani marehemu hakuonesha dalili zozote za kuwa na mipango ya baadaye na Lulu,” alisema Seth.
Kuhusu madai ya Kanumba kumpachika mimba Lulu kisha kumtaka aitoe, Seth hakukubali wala kukataa, badala yake alisema kwa kifupi: “Kanumba aliheshimu na kuwapenda sana watoto na alikuwa akiniasa juu ya kutotoa mimba.”

Posted by Unknown on 11:42 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added