|

Uwoya na Flora Mvungi Wapakana Kisa H-Baba




MASTAA wawili wanaokimbiza kwenye sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Flora Mvungi hivi karibuni wamevunjiana heshima kisa kikiwa ni msanii wa Bongo fleva, Hamis Ramadhani Baba ‘H. Baba’ Risasi Jumamosi linakujuza.
Akizungumza na gazeti hili, Flora ambaye anatoka na H. Baba hivi sasa, alionesha kukasirishwa na kitendo cha Uwoya kumtolea kashfa mwanaume wake huyo mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kwa kusema kuwa hayajui mapenzi.
HUYU HAPA UWOYA 
Katika mahojiano aliyofanya na jarida moja la burudani hivi karibu, Uwoya bila ya kuumauma maneno, alishusha tuhuma nzito kwa H. Baba ambaye alikuwa mwandani wake wa zamani na kumchana kwamba ni ‘mbumbumbu’ anapofika kwenye kiwanja cha sita kwa sita ndiyo sababu penzi lao likavunjika.
FLORA ANATIRIRIKA
“Anadai H. Baba hajui mapenzi wakati miye ndiyo nimefika, ananiridhisha vya kutosha! Yeye ndiyo hajui mapenzi ndiyo maana hakai na wanaume kila siku anamzungumzia H. Baba. Atakuwa bado anamtaka angekuwa muwazi, asingekuwa anamzungumzia kila siku.
“Kuna raha anazozikumbuka ndiyo maana anaongea sana. Wanaume wote aliotoka nao mbona hawazungumzii? Aseme anachotaka asizunguke,” alisema kwa hasira.
Frola anadai kuwa Uwoya roho inamuuma kwa kuwaona wawili hao wanavyopendana, kama vile haitoshi Frola alisema kuwa Uwoya hawezi kuishi na mwanaume ndiyo maana hata ndoa yake imemshinda.
“Si aliolewa na anayedhani anajua mapenzi, mbona kashindwa kudumu naye?” alihoji Frola.
NI KWA NINI H. BABA?
Kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita inaonesha, Uwoya aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na H. Baba wakamwagana, hivyo imedaiwa kuwa hafurahi kumuona Flora akifaidi mapenzi motomoto ya H. Baba.
KUMBE NI VITA YA MUDA MREFU
Mbali na Uwoya ‘kumvua’ vibaya H. Baba kwenye jarida hilo kwamba hajui mapenzi, chanzo makini kimeeleza kuwa mara kwa mara Uwoya amekuwa akimtupia vijembe vya dharau Flora kwamba amejiweka kwa mtu ambaye hajui mapenzi.
“Siyo mara moja wala mara mbili, Uwoya anawadharau sana H. Baba na Flora hata hivi majuzi amewachana redioni,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini.

Posted by Unknown on 8:54 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added