Timu ya Gyan Asamoah yamwaga Sh 160m
Kiungo mpya wa Yanga, Nizar Khalfan.
Na Saleh AllyKlabu ya Al Ain ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), imesema ipo tayari kumsajili kiungo mpya wa Yanga, Nizar Khalfan, kwa kutoa dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 160), bila kuchelewa.
Al Ain ndiyo timu ya Uarabuni anayoichezea mshambuliaji nyota raia wa Ghana, Asamoah Gyan ambayo ilimchukua kwa mkopo kutoka Sunderland ya England na kulipa ada ya pauni milioni 6 (zaidi ya Sh bilioni 15).
Mmoja wa maofisa wa Al Ain, Mohammed Ismail, ameliambia Championi Jumatano kuwa wamefanya mawasiliano na Yanga kuhusiana na kumtaka Nizar.
“Tumewaambia kuwa tunamhitaji na tupo tayari kulipa kiasi hicho, wakiwa tayari basi tutampokea. Tunahitaji viungo ili wasaidie mashambulizi, pale mbele tunaye Gyan Asamoah, nafikiri unajua hilo,” alisema Ismail.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa tayari suala hilo limewasili ndani ya Yanga na Nizar amekwishapewa taarifa lakini inaonekana hana mpango wa kuiacha Yanga ambayo amejiunga nayo hivi karibuni baada ya kuachwa na Klabu ya Philadelphia Union ya Marekani.
“Kweli tumepata hayo maombi, lakini ni suala ambalo lipo chinichini. Zaidi tunaangalia kwanza, maana Nizar tunamhitaji na hatujui yeye anahitaji nini, lakini jamaa wameahidi kutoa mshahara mnono,” kilieleza chanzo.
Al Ain ni miongoni mwa timu tajiri na hivi karibuni ilitangaza nia ya kumbakiza Asamoah kwa kutoa ofa ya euro milioni 60 (Sh bilioni 120) na mshahara wa euro 250,000 (Sh milioni 500) kwa wiki.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Nizar alisema alipata taarifa kuhusiana na dili hilo lakini hajakaa chini na viongozi wake.
“Kweli nilisikia taarifa kuhusiana na hilo, nimeambiwa na mmoja wa viongozi lakini haikuwa rasmi sana,” alisema Nizar ambaye alisisitiza asingeweza kulizungumzia zaidi hadi atakapopata taarifa za uhakika.
Iwapo Nizar atakubali kuondoka na Yanga ikaona hakuna ‘gogoro’, mchezaji huyo atapata nafasi ya kucheza kikosi kimoja na Asamoah.
Al Ain inaona sahihi kumbakiza Asamoah baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa wa 10 wa ligi ya UAE huku akiwa amefunga mabao 22 katika mechi 18 alizocheza katika mashindano yote.
Klabu hiyo imekuwa ikitaka kujiimarisha zaidi na wachezaji kadhaa nyota kama Abedi Pele (Ghana), Hossam Hassan (Misri), Mustapha Hadji (Morocco),