STAA BONGO MOVE APIGWA STOP KUIGIZA
Nyota kutoka tasnia ya filamu Bongo Skyner Ally huenda asionekane tena kwenye ulimwengu wa move kufuatia kupigwa stop kushiriki katika kuigiza.
Stori 'under carpet' ambazo Teentz.com imezinyaka kutoka kwa mmoja wa wapambe wa mwigizaji huyo aliyeng'arisha nyota yake kupitia filamu ya 'SECOND WIFE' iliyopikwa na mkali Ray Kigosi, zinasomeka kuwa Skyner amepigwa stop na wazazi wa upande pili (wakwe) ili aweze kulea vizuri mtoto wake badala ya kutumia muda mwingi akiwa kambini na waigizaji wengine kwa ajiri ya kurekodi 'muvi'.
"amezuiwa, na sijui kama ataruhusiwa kipindi cha karibuni na huenda ikawa moja kwa moja kwani ameambiwa atulie alee familia na mtoto wake, alisema mpambo huyo.
"kuona hivyo, Teentz ilimvutia waya msanii huyo na majibu yake yakawa hivi: unaweza kuona nimezuiwa lakini kwangu mimi sijachukulia hivyo kilichopo ni kuwa nimetulia kwanza nilee mtoto wangu na familia pia, kwa sasa nipo Tanga nimekuja kusalimia ndugu na baada ya muda nitarejea Dar halafu ndiyo nitatoa jibu kamili kama nitaendelea ama la" alisema Skyner.