|

Fani Ya Umodo na Ushoga


.FANI ya u-modo (mitindo) ambayo awali ilionekana kuwa nyuma nchini Tanzania, sasa imeshika kasi baada ya akina dada warembo na wakaka watanashati kujikita huko.
Ma-miss Tanzania, Jokate Mwegelo, Victoria Martin, Nasreen Karim, Miriam Odemba, Happiness Magese na Fideline Iranga, ni miongoni mwa mifano mikubwa ambapo sasa wameamua kujidhatiti kwenye fani hiyo ili kuikuza hapa Bongo.
Kwa upande wa wanaume, Kenedy Victor ‘Kenny’, Mister University 2001, Matukio Chuma, Martin Kadinda, Ahmed Mwinyigumba ‘Mwinyi’ na Ally Remtulah (pia mbunifu wa mavazi) ni vijana wa Bongo walioegemea fani hiyo.
Mdogo wa mwanamitindo aliyepiga kambi Afrika Kusini, Dayana Nells, Wancy Nells (pichani) naye ametumbukia kwenye shughuli hiyo akifanya kazi zake na Kampuni ya Mitindonite Afrika yenye makazi yake Bongo na nje ya nchi.
Mwenyewe anasema: “Kwa kweli Bongo kwa sasa tuko juu, uanamitindo umefika mahali pa kuwa ajira si kama zamani. Nawapongeza wote wanaotupa sapoti hasa Global Publishers. Nawasihi vijana wa kiume kama mimi wajitokeze kwa wingi kwani kwenye mitindo hakuna ushoga kama baadhi ya watu wanavyovumisha.”
Wancy alitoa ushauri kwa wanamitindo kuunda chama imara kwa ajili ya kutetea maslahi yao ambapo alidai kwa sasa wengi, ukiacha wakongwe, hawajitambui.

Posted by Unknown on 9:45 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added