Diamond Apagawisha Songea-Show Yavunja Record
SHOO ya nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo Naseeb Abdul 'Diamond' imeingia katka kitabu cha matukio yaliyokusanya watu wengi zaidi katika historia ya mji wa songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Akizungumza na Teentz.com mapema leo Mkurugenzi wa Jambo Lee Club ambayo iliratibu ziara nzima ya mwanamuziki huyo amesema kuwa shoo ya Diamond imevunja rekodi na kuingia kwenye kumbukumbu za watu kwa kujaza watu wengi na pia ikiwa ni shoo pekee iliyokuwa na msismko mkubwa kuliko hata inavyokuwa wakati wa michezo ya soka inayozihusisha timu kubwa na Simba na Yanga zinapokuja kucheza Songea.
"Shoo imefunika hakika haijawahi kutokea, watu kujaa kwa wingi kiasi kile katika shoo za muziki hii imevunja rekodi, kwa kweli kama waratibu tumefarijika sana kuona watu wamejitokeza kwa wingi, kwani hatukutegemea ingawa msisimko uliokuwepo kabla ulikuwa mkubwa kuliko hata ule unaokuwepo wakati Simba na Yanga zikija kucheza hapa Songea" alisema Mukugenzi huyo.