|

Stars kufanya kama Ivory Coast



KOCHA wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema atafanya kama walivyofanya Ivory Coast waliotumia vizuri faida ya uwanja wa nyumbani kuibuka na ushindi, akitarajia kufanya hivyo dhidi ya timu ya Taifa ya Gambia inayotarajia kuwasili nchini wakati wowote kuanzia leo.

Stars itashuka dimbani Jumapili wiki hii kuikabili Gambia huku ikiwa na majeraha ya kipigo cha mabao 2-0 toka Ivory Coast katika mechi yao ya kwanza kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam mara baada ya mazoezi ya asubuhi kwenye Uwanja wa Karume, Poulsen alisema amekiandaa kikosi chake kupata ushindi kwenye mchezo huo Uwanja wa Taifa.

Kim alisema kiwango walichoonyesha wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Ivory Coast kimemtia moyo na ana hakika watafanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Gambia.

"Wachezaji wana moyo hata kwenye mazoezi wakionyesha uwezo mzuri, lakini haina maana mchezo wetu utakuwa rahisi bali tutacheza kwa kujituma zaidi na kuepuka kufanya makosa yaliyotugharimu Ivory Coast," alisema Kim.

Wakati huohuo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo, ambapo kiingilio cha juu kitakuwa Sh30,000 na cha chini Sh3,000.

Jukwaa la rangi ya Machungwa, Sh5000, VIP C 10,000, VIP B 20,000 na VIP A 30,000. Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa Jumamosi.

Posted by Unknown on 3:06 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added