|

Qeeny Suzi na Sharapova Wazichapa Kavu Kavu


WANENGUAJI mashuhuri Bongo, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ na Asha Said ‘Sharapova’ wa African Stars ‘Twanga Pepeta’, wamezichapa kavukavu, Ijumaa Wikienda lina kisa kamili.
NI MAISHA CLUB
Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita ndani ya New Maisha Club, Masaki jijini Dar es Salaam baada ya wawili hao kukutana kwenye burudani iliyoporomoshwa na Twanga Pepeta.
Akiwa ukumbini humo, Queen Suzy alitimba kwenye jukwaa la Twanga Pepeta akiwatunza wanenguaji wa kike kwa kazi waliyokuwa wakiifanya stejini ambapo aliwatunza wote isipokuwa Sharapova.
Baada ya wanenguaji hao kushuka jukwaani, Sharapova alionekana akielekea ‘toileti’ ambapo Queen Suzy naye alielekea huko akiwa na kundi kundi la wasichana wanne na baada ya kufika huko ndipo tafrani ikatokea na kuchapana makofi kwa kwenda mbele.
Mtiti huo ulichukua takribani dakika 10 na baadaye Sharapova alionekana akitokea msalani na kupanda stejini kunengua ambapo Queen Suzy alihamishia ugomvi kwa mhudumu wa baa ya Sharapova (aliyetajwa kwa jina moja la Angela) na kuwaita mabaunsa ambao walimdaka Angela na kumtoa nje ya klabu.
SHARAPOVA NYUMA YA NONDO
Baada ya shoo kumalizika, Sharapova alichomoka na kwenda kumfuatilia Queen Suzy na Angela ambapo tayari walikuwa wameshalikimbiliza soo polisi baada ya Queen Suzy kutoka nduki na kumuita askari wa kituo cha Polisi cha Kati (Central) ambapo Sharapova alikamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu hadi alipochomolewa na mchumba’ke, Jumanne Said ‘J4’ alfajiri.
KISA NI NINI?
Queen Suzy na Sharapova wamekuwa kwenye bifu la muda mrefu kisa kikifahamika kuwa ugomvi wa kugombea mwanaume ambaye ni aliyekuwa rapa wa FM Academia, Aimerichard Mwamba ‘G-Seven’.

Posted by Unknown on 1:34 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added