|

Mapacha waahidi kumsaidia Dogo Janja apate haki yake


Kundi la Hip-hop linaloundwa na mapacha K na D wa Maujanja Saplayaz limeahidi kufanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Diogo Janja aliyefukuzwa Tip Top Connection na kurudi Arusha wiki hii anapata haki yake.
Jana kupitia Capital Fm, Kulwa ambaye ni mmoja wa mapacha hao amesema sio haki msanii huyo mwenye umri mdogo kurudi nyumbani bila chochote licha ya kuliingizia kundi hilo hela fedha za kutosha kutokana na show alizokuwa akifanya.
“Haki ya Dogo Janja iko wapi? Kama anarudi Arusha bila ya chochote! Madee imefika mahali lazIma watu wajue ukweli maana maongezi yako kwenye vyombo vya habari yanagongana. Kama kuna unyonyaji ulikuwa unaendelea basi watanzania wajue na hatma ya huyo dogoifikiwe na apewe haki yak. Tumeshoshwa na unyonyaji magenge ya mwenge,” aliandika K kupitia Facebook wiki hii.
Dogo Janja alirudi kwao Arusha Alhamis ya wiki hii baada ya uongozi wa Tip Top Connection kusema kuwa alilewa sifa, kuendekeza starehe na utoro shuleni.
Hata hivyo yeye alisema ameamua kuondoka baada ya kuishi maisha ya tabu, kudhulumiwa haki yake na kufanywa kama kitega uchumi cha kundi hilo.

Posted by Unknown on 2:19 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added