Banda la Kanumba Saba Saba Jul 2012
Wakati huu ambapo maonyesho ya sabasaba yanakaribia kuanza Dar es salaam familia yake imeamua kuchukua banda maalum kwenye viwanja vya saba saba kwa ajili tu ya kuendelea kumuenzi Marehemu Kanumba.
Seth ambae ni Mdogo wake waliekua wakiishi pamoja Sinza Dar es salaam amesema ni banda la Kanumba litakalokua na Nguo zenye alama alizokua anazitumia Kanumba ikiwa ni pamoja na jina na ujumbe, kutakua na picha zilizo kwenye frame za Kanumba zinazomuonyesha toka akiwa utotoni, pia vikombe, kanga, bazee na vitu vingine vingi vyenye alama na picha za Kanumba.
Seth amesema Mama mzazi wa Kanumba pamoja na watu aliokua akifanya nao kazi Kanumba watakuwepo kutoa maelezo mbalimbali kuhusu Kanumba na kazi zake.