Update:Beef la Mike T na Eryne Epidu lageukia kwenye uchawi
Ugomvi kati ya Waliokuwa wamiliki wenza wa kampuni ya video ya Shobiz Defined Mike T na Eryne Epidu umechukua sura mpya baada ya Eryne kumshutumu Mike T kuwa anataka kumroga.
Eryne amemshushia Mike tuhuma hizo nzito usiku wa kuamkia leo kupitia Facebook.
“Usiku wa leo (May 24), Mike tee amebeba watu wasio julikana kawaleta nyumbani Kimara ati, waje kusearch nyumba yangu. Watu 6 wamekuja bila kibali cha polisi na wanajidai ni polisi,” ameandika Eryne.
Ameongeza, “walitaka kuweka madawa au unga. Bahati mbaya wamekuta watu wako steady.”
“I wish I knew people but I don’t,” Eryne aliendelea. “Jealousy na kutosoma. Maana taarifa ninazopata kutoka Dar eti zina uchawii ndani yake. Shetani mbaya nyie, ameanza kumdhalilisha mshikaji hadharani kwa kumfanya kama mwehu. Ndugu zake walio msindikiza usiku wa leo wamesikika wanasema anarogwa akiwemo shangazi yake.”
Eryne ambaye kwa sasa amerejea kwao nchini Uganda, anadai Mike alimlengesha kwa maofisa wa uhamiaji ambao walimtimua nchini.