|

DOGO JANJA: NIOKOENI KWENYE NJAA


Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.
Dogo anayekimbiza kwenye Hip-hop Bongo, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amewaomba mashabiki wanunue albamu yake ya Mtoto wa Uswazi inayokimbiza sokoni ili wamuokoe kwenye njaa.
Akizungumza na mtandao huu jana, Dogo Janja alisema mzigo huo ulikamilika miezi sita iliyopita na unapatikana madukani ambapo ukibahatika kupata nakala yako utasikia ngoma kali zaidi ya 10 zikiwemo Anajua, Mtoto wa Uswazi, Mimi ni Noma na Siri Zao.

“Nawaomba mashabiki wangu wanunue kwa wingi, itanipunguzia njaa kwani shoo pekee hazitoshi. Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kuipata wanipigie kwa namba 0655 336644,” alisema Dogo Janja.

Posted by Unknown on 4:06 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added