|

BARNABA ATAJA IDADI YA WAPENZI ALIOKUA NAO KABLA YA HUYU!



Feb 14 siku ya wapendanao, Staa wa single mpya ya GUBEGUBE, Barnaba (21) amekubali kwamba kabla ya kumpata wake wa sasa alishawahi kuwa kwenye mahusiano na wasichana wengine watatu tofauti na amejifunza vya kutosha.
B boi (21) amesema kilichomfanya aridhike na mpenzi wake wa sasa ni akili nzuri ya maisha aliyonayo tofauti na wasichana waliopita.
ameamplfy zaidi kwamba “wasichana waliopita walikua hawayajui maisha, unaweza kumpa elfu 50 akaimalizia saloon kupaka rangi kucha na kutengeneza nywele lakini huyu wa sasa unaweza kumpa pesa ndogo na akaitumia vizuri mkapata chakula siku nzima, Nampenda sana”
kosa kubwa ambalo huwaachanisha wapenzi wengi ni kukosekana kwa uaminifu kati yao, lakini kwa Barnaba hajawahi kukutana na hiyo ishu, sababu kubwa iliyomfanya aachane na wapenzi wake ni hiyo ya wao kujifanya wa mjini.
Barnaba na mpenzi wake wa sasa wameanza kuishi pamoja zaidi ya miezi tisa iliyopita, ambapo siku yoyote kuanzia leo wanaweza kupata mtoto wao wa kwanza ambae hawakumtarajia lakini wamekubali kilichotokea”
Habari kwa hisani ya : http://millardayo.com/

Posted by Unknown on 1:53 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added