|

Watangazaji wa kike waunda kundi la kusaidia


Gea Habib.
Na George Kayala
Watangazaji wa kike kutoka vituo mbalimbali vya runinga na redio nchini, wameunda kundi litakalojulikana kama Umoja wa Watanzangaji Marafiki Tanzania ambalo litakuwa na kazi ya kuwasaidia wanawake wasiojiweza.
Habari zilizovuja kutoka miongoni mwa wanaounda kundi hilo zilisema kuwa, kundi hilo litaundwa na wanaharakati kama Maimartha Jesse, Sauda Mwilima, Zamaradi Mketema, Dina Marios, Gea Habib na wengine wengi.
Mpenyesha habari huyo aliendelea kusema kuwa, kundi hilo litakuwa na jukumu la kutoa mitaji kwa vikundi vya wanawake wasiojiweza na kutoa elimu ya ujasiriamali.
Baada ya kuzidaka habari hizo, gazeti hili lilifanya juhudi za kumsaka mmoja wa wanaodaiwa kuunda kundi hilo, Maimartha ambaye alikiri kuundwa kwa kundi hilo na wanaharakati hao na kudai kuwa bado mapema kulizungumzia kwa undani zaidi.
“Ni kweli kundi hilo lipo lakini bado mapema sana kulizungumzia kwani kuna mambo bado tunakamilisha ndipo tutaweka kila kitu hadharani,” alisema Maimartha.

Posted by Bongo Flavor on 2:15 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added