|

Wema anunuliwa gari baada ya kuachana na Diamond

Msanii wa filamu Bongo asiyeishiwa na matukio, Wema Sepetu amenunuliwa gari la kifahari na ndugu zake huku ikidaiwa kuwa ni pongezi kwa kuachana na mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.


Wema hivi karibuni aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, gari hilo la shilingi milioni 35 aina ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T 211 BXR, amenunuliwa na mama yake pamoja na ndugu wengine kufuatiakufurahishwa na uamuzi mgumu aliouchukua.

Awali kulikuwa na tetesi kuwa, gari hilo analotumia mrembo huyo kwa sasa amehongwa na mwanaume aliyechukua nafasi ya Diamond.
kazidi kudaiwa kuwa, lengo la mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clemence kumnunulia Wema gari ni kumwepusha na vishawishi kutoka kwa wanaume mapedeshee.
“Lile gari analotembelea Wema kanunuliwa na yule jamaa yake wa sasa, si unajua tena mtoto mzuri kama yule hawezi kutumia daladala au teksi?” kilishadadia chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Wema.
Wema afunguka
Akizungumzia madai hayo, Wema alisema wanaoamini amehongwa gari hilo wanakosea kwani ukweli ni kwamba amenunuliwa na ndugu zake kama zawadi.
“Najua kila mmoja atakuwa na lake la kusema juu ya hili gari ninalotumia kwa sasa, ukweli ni kwamba nimenunuliwa na mama na ndugu zangu wengine baada ya kutoka kwenye kashikashi zito na Diamond.
“Na mimi zaidi ya kuwashukuru pia naahidi kutowaangusha na nitajitahidi kutowakosea kwa namna yoyote ile,” alisema Wema.
Wema alikuwa mpenzi baadaye mchumba wa Diamond lakini hivi karibuni wawili hao walitibuana huku pia kukiwa na madai kuwa baadhi ya ndugu wa Wema


Habari kwa hisani ya:http://www.g5click.com/

Posted by Bongo Flavor on 3:26 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added